Na
Rajabu Singana. Mahakama Kuu Mbeya
Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba amekutana na
uongozi wa Benki ya NMB na kufanya mazungumzo juu ya uanzishwaji wa huduma za Kibenki
katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya linalotoa huduma kwa Mahakama Kuu, Mahakama
ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya.
Mhe. Makaramba alikutana na uongozi huo mapema
Agosti 28, na kuwaeleza viongozi hao kuwa Mahakama ipo katika maboresho
makubwa ya huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano (2015-2020)
unaolenga kumsogezea mwananchi huduma.
Kutokana
na changamoto ya kufanya malipo ambayo wamekuwa wakiipata wananchi Mhe.
Makaramba aliwaomba NMB kusogeza huduma zao katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya.
Akichangia
katika mazungumzo hayo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Straton Chilongola alisema kwa sasa
Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Mawakala ambao hufanya
kazi za Kibenki.
Bw.
Chilongola aliongeza kwa kusema kwamba watafanya utaratibu wa kuanzisha ‘Cash
Collection Point’ kwa ajili ya wananchi kufanya malipo ya Huduma za Mahakama.
Meneja
wa Wakala wa Benki wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Respicious Denis
aliongeza kuwa kwa sasa benki ya NMB imekuwa ikifanya vizuri kwa kutumia
Mawakala kwenye malipo na makusanyo mbalimbali ambapo tayari baadhi ya taasisi
za serikali zinatumia huduma hiyo.
Alizitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na TRA, Idara
ya Maji Mbeya na walitumia mfumo huo katika makusanyo ya NaneNane mwaka huu.
Ifahamike
kwamba baada ya ukarabati mkubwa wa jengo la Mahakama Kuu Mbeya, Uongozi wa
Mahakama ya Tanzania ulifikia maamuzi ya kulifanya jengo hii kuwa Kituo
Jumuishi cha kutoa huduma za Mahakama.
Viongozi
wa Mahakama Kanda ya Mbeya (kushoto) wakiwa katika majadiliano na Viongozi wa Benki ya
NMB, majadiliano juu ya uanzishwaji wa huduma za kibenki ili kuwarahishia
wateja wanaofika katika Mahakama hiyo.
Mjumbe kutoka NMB akichangia jambo katika majadiliano.
Picha ya pamoja baada ya majadiliano, (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya.
(Picha na Rajabu Singana, Mahakama Kuu, Mbeya)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni