Alhamisi, 9 Agosti 2018

MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YASHIRIKI KUTOA ELIMU YA SHERIA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA-NANE NANE, 2018


Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora imeshiriki katika Maonesho ya Wakulima Nane Nane ya mwaka 2018, lengo la maonesho hayo ni kutoa elimu ya sheria kwa Wananchi na Wadau muhimu wa Mahakama.

Katika utekelezaji Mpango Mkakati wa Mahakama, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetumia fursa hii kutekeleza nguzo ya tatu ya mpango mkakati huo ambayo ni Kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau.

Katika Maonesho hayo, Mahakama imetoa elimu kwa umma kuhusu huduma mbalimbali za Kimahakama na maboresho yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama.

Katika Maonesho hayo, Mahakama imeelimisha umma kwa kuonesha  matumizi ya Tehama katika utoaji haki Mahakamani.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za ushiriki wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora katika Maonesho hayo.

Baadhi ya Wananchi waliotembelea banda la Mahakama katika kilele cha Maonesho ya Wakulima, Nanenane wakipatiwa huduma.
Bi. Mwanaenzi Chuma akifafanua kwa wananchi kuhusu matumizi ya TEHAMA Mahakamani.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya Tabora, Mhe. Seraphine Nsana akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari waliotembelea katika banda hilo.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Tabora Mjini, Mhe. Judica Nkya akifafanua jambo kwa mteja aliyetembelea katika banda la Mahakama. 
Mahakama ni mmoja wa Wadau walioshiriki kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika viwanja vya Ipuli mkoani Tabora.

(Picha na Aisha Abdallah, Mahakama Kuu-Tabora)
 
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni