Na
Festo Sanga, Mahakama ya Mkoa- Kigoma
Mtendaji
Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Husssein Kattanga amefanya ziara mkoani Kigoma
na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu lililoanza kujengwa
rasmi tarehe Oktoba 28, 2017 chini ya mkandarasi Masasi Construction Co Ltd.
Ujenzi
huo wa Jengo la Mahakama Kuu utasogeza huduma za Kimahakama karibu na wananchi wa
Mkoa huo kwani wamekuwa wakisafiri kutoka Kigoma kwenda Tabora kufuata huduma
za Mahakama Kuu.
Katika
ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama alipata fursa ya kutembelea mahakama ya Wilaya
Kasulu na kukagua ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu inayotegemewa kumalizika
mwezi April 2019 chini ya Mkandarasi M/S Molad Tanzania LTD.
Ujenzi wa Mahakama mbalimbali nchini unalenga
katika kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi na vilevile ni
utekelezaji dhahiri wa nguzo ya pili ya mpango mkakati wa Mahakama (2015/2016-2019/2020)
ya upatikanaji wa haki kwa wakati.
Aidha
ujenzi wa jengo hilo la Mahakama na unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019 utawezesha
uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali na kuimarisha matumizi ya vifaa
vya TEHAMA katika huduma ya utoaji haki.
Hali
ya jengo la Mahakama Kuu kanda ya Kigoma lilipofikia.
Mtendaji
Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma Bw. Moses Mashaka akiwasilisha taarifa ya
utendaji kazi mbele ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga
na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama, Bw Hussein Kattanga (wa kwanza kulia) akikagua kiwanja
kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Wilaya Buhigwe ikiwa ni muendelezo wa
kusogeza huduma kwa wananchi mkoani Kigoma.
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Kattanga akitoa maelekezo alipotembelea ujenzi wa
Mahakama ya Wilaya Kasulu mkoani Kigoma katika ziara yake aliyofanya Wilayani
humo Agosti, 08, 2018.
Picha
ya pamoja ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama , viongozi wa Mahakama Mkoa wa Kigoma na
wakandarasi wa Masasi Construction wakiwa mbele ya jengo la Mahakama Kuu Kanda
ya Kigoma linaloendelea kujengwa.
(Picha na Festo Sanga, Kigoma)
(Picha na Festo Sanga, Kigoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni