Jumatatu, 6 Agosti 2018

MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA YA TANZANIA AKAGUA UJENZI WA MAHAKAMA KUU MARA

  Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Mara kama linavyoonekana hivi sasa, linaendelea kujengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia. Jengo hili pamoja na lile la Mahakama Kuu kanda ya Kigoma yanatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili, 2019 na kufanya idadi ya kanda za Mahakama Kuu kufikia 16 nchini.

 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Bw.Hussein Kattanga akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wengine wa Mahakama pamoja na Mkandarasi alipotembelea kukagua ujenzi wa jengo hilo unaoendelea hivi sasa mjini Musoma.

  Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Bw.Hussein Kattanga akimuelekeza jambo Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi.
  Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Bw.Hussein Kattanga akielekeza jambo alipotembelea ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mara unaoendelea. Wa kwanza kushoto mwenye kofia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Leonard Magacha.
 

 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Bw.Hussein Kattanga akisaini kitabu cha wageni.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni