Jumatatu, 6 Agosti 2018

WATUMISHI WA MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA ARDHI WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SARATANI

  Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Leila Mgonya (Mwenye miwani kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni za Ardhi na Biashara waliowatembelea watoto wenye Saratani na kutoa misaada katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi pamoja na Divisheni ya Biashara mwishoni mwa wiki walitoa msaada wa vifaa tiba na dawa kwa ajili ya watoto wenye ugonjwa wa Saratani walioko kwenye Wodi ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Watumishi hao waliwatembelea watoto hao kwa lengo ka kuwajulia hali,  kuwafariji kuwaombea na kuwapatia misaada hiyo.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni pamoja na dawa kama zilivyopendekezwa na hospitali hiyo, viti maalum kwa wagonjwa wasiojiweza (wheelchair), pamoja na  maji ya kunywa.
Baada ya kuwasilisha misaada hiyo, wazazi wa watoto hao walishiriki katika sala ya pamoja iliyofanywa na Watumishi hao wa Mahakama.

 Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Leila Mgonya akiwa na watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni za Ardhi na Biashara wakitoa msaada kwa watoto wenye Saratani katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Baadhi ya vifaa Tiba vilivyotolewa
  Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Leila Mgonya (mwenye nguo nyeupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Divisheni za Ardhi na Biashara waliowatembelea watoto wenye Saratani na kutoa misaada katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 
 Watumishi wakifurahia jambo.

(Picha na Dhilon John- Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni