Na
Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya
Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali vyeo na kufanya kazi kama timu moja, kupendana na kufuata C tatu yaani ‘Coordination, Cooperation na Consultation’ ili kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba alipokuwa akiongea na Watumishi wa Kanda hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi Agosti, 15 2018, katika ofisi za Mahakama Kuu mkoani Mbeya.
Mhe. Jaji Makaramba alisisitiza viongozi wa ngazi ya juu ya Kanda hiyo yaani Jaji Mfawidhi, Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama kufanya kazi kwa kufuata kile alichokiita ‘utatu mtakatifu’.
Aidha,
pamoja na mambo
mengine, Mhe. Makaramba alisisitiza juu ya nidhamu na uadilifu wa watumishi wa Mahakama huku akikemea
Watumishi kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kwa pamoja kuweza kufikia malengo ya
Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Mahakama.
“Mtumishi
akikamatwa kwa tuhuma za rushwa nitamsindikiza mwenyewe hadi TAKUKURU nikifika
nawakabidhi wamalizane naye wenyewe” alisema Jaji Mfawidhi huyo.
Mhe.
Makaramba vilevile aliupongeza uongozi
wa Mahakama ya Tanzania kwa kazi nzuri ya ukarabati wa jengo la Mahakama Kuu
Mbeya ambalo pia hutumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi pamoja na Mahakama ya
Wilaya Mbeya na kuwataka Watumishi kulitunza vyema jengo hilo pamoja na vitendea
kazi vya kisasa vilivyomo.
Aidha; Mhe. Jaji Makaramba alitoa
maagizo ya kuwa na mpango kazi wa Kanda ambao utaenda sambamba na mpango
Mkakati wa Mahakama kitaifa ili kutengeneza mazingira mazuri na wezeshi ya kuwahudumia wananchi.
Aliongeza
kwa kusema kwamba yupo tayari kutoa mchango wake kadri akatavyojaaliwa na
Mwenyezi Mungu vile vile ataendelea kujifunza kutoka kwa watumishi wa Kanda ya
Mbeya mambo mbalimbali yatakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi
kwa wakati.
Viongozi
na Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya wamempokea Mhe Robert Makaramba
ambaye amehamishiwa mkoani humo kuwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo kujaza nafasi ya Jaji Mfawidhi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwepo kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Pamoja
na mapokezi hayo, makabidhiano ya ofisi yalifanyika kati ya Mhe. Makaramba na
Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira akimwakilisha Mhe. Kaimu Jaji mfawidhi ambaye
alipatwa na udhuru.
Katika
hafla hiyo Mhe. Dkt. Levira alisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi ikijumuisha
mambo muhimu ikiwepo eneo la utawala wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa kueleza
kuwa Kanda ya Mbeya inajumuisha Mikoa ya Mbeya na Songwe.
Vilevile
katika taarifa hiyo kulikuwa na taarifa ya hali ya mashauri, hali ya watumishi,
hali ya miundombinu, hali ya fedha na
hali ya vyombo vya usafiri.
Mhe
Jaji Makaramba akisaini kitabu cha wageni.
Mhe.
Dkt. Levira akisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi.
Mhe.
Makaramba akipokea taarifa ya makabidhiano ya ofisi kutoka kwa Mhe Dkt. Levira.
Watumishi
wakimsikiliza Mhe. Jaji Makaramba, Mhe. Makaramba alipata pia fursa ya kuzungumza na Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya.
Jaji
Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na
baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya, (wa tatu kushoto) ni Mhe. Jaji
Paul Joel Ngwembe, (wa pili kulia) ni Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili-Mahakama Kuu,
Kanda ya Mbeya, Mhe. George Herbert, wa pili kushoto ni Naibu Msajili,
Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. William Mutaki na wa kwanza kushoto ni
Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete.
Mhe Makaramba akipanda mti wa kumbukumbu.
Mhe
Dkt. Levira akipanda mti wa kumbukumbu.
Mhe
Ngwembe akipanda mti wa kumbukumbu.
(Picha na Rajabu Singana, Mahakama Kuu, Mbeya)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni