Jumatatu, 13 Agosti 2018

MANAIBU WASAJILI WA MAHAKAMA WAKUMBUSHWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU

Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Edson Mkasimongwa (kulia )akizungumza jambo katika kikao kazi cha  Jaji Kiongozi na Manaibu Wasajili wa Mahakama Kuu Masijala  Kuu, wakiwemo Manaibu Wasajili wa Kanda ya Dar es Salaam na Divisheni zake, kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu Mhe.Isaya  Arufani.  Jaji Mkasimongwa  na Jaji  Arufani wamemwakilisha Jaji Kiongozi, kwenye kikao hicho.
Katika kikao hicho cha Mhe. Jaji Kiongozi ambaye amewakilishwa na Waheshimiwa Majaji hao, amewataka Manaibu Wasajili kuwa Wabunifu, hodari na Jasiri katika utendaji wao wa kazi.

Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.Isaya  Arufani (kushoto) akizungumza jambo katika kikao kazi cha  Jaji Kiongozi na Manaibu Wasajili wa Mahakama Kuu Masijala  Kuu, Manaibu Wasajili wa Kanda ya Dar es Salaam na Divisheni zake. Jaji Arufani  na Jaji  Mkasimongwa  wamemwakilisha Jaji Kiongozi, kwenye kikao hicho ambaye hayupo pichani.
Manaibu Wasajili wa Mahakama Kuu Masijala  Kuu na Manaibu Wasajili wa Kanda ya Dar es Salaam na Divisheni zake wakiwa katika kikao kazi kati yao na Jaji Kiongozi ambaye hayupo pichani.

Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba pamoja Manaibu Wasajili wenzake wakiwa katika kikao hicho.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Safina Simfukwe akiuliza jambo katika kikao  kazi hicho.
Naibu  Msajili Mhe. Angela Teye Mahakama Kuu, Kitengo cha Usuluhishi akizungumza jambo katika kikao kazi hicho.

(Picha na Magreth Kinabo)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni