Jumanne, 28 Agosti 2018

WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU ZA NDANI WA MAHAKAMA WAPATIWA MAFUNZO


 Na Rashid Omar, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Pwani


Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za  ndani wa Mahakama wametakiwa  kuongeza juhudi zaidi katika  ufanyaji kazi wao ili kuipeleka Mahakama katika uelekeo sahihi.

Hayo yalisemwa mapema Agosti 27 na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Dodoma, Mhe. Ignas Kitusi alipokuwa akifungua rasmi Mafunzo ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za ndani wa Mahakama yanayofanyika Mkoani Dodoma.

Mh. Jaji Ignas Kitus. alisema kuwa nia ya mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo zaidi Wahasibu na wakaguzi hao katika kuongoza na Kudhibiti fedha zinazotolewa katika miradi mbalimbali ya Mahakama na Wafadhili.

Katika hotuba yake kwa washiriki wa semina hiyo, Jaji Mfawidhi huyo aliwakaribisha  washiriki jijini Dodoma na kuwapongeza kwa kupata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo.

“Mnatoka katika vituo mbalimbali vya kazi nchi nzima, hivyo ni matarajio yetu kwamba mtatumia vyema mkusanyiko huu kubadilishana uzoefu mlio nao ili kuipeleka Mahakama katika uelekeo bora na sahihi ” alisisitiza Mhe. Jaji Kitusi.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma Mh. jaji Ignas Kitus akifungua rasmi Mafunzo kwa Wahasibu na wakaguzi wa  ndani wa hesabu za Mahakama jijini Dodoma.

Sehemu ya  Washiriki wa  Mafunzo kwa Wahasibu na wakaguzi wa  ndani wa hesabu za Mahakama wakifuatilia kwa makini  mafunzo hayo.
Mmoja wa wawezeshaji wa Mafunzo kwa Wahasibu na wakaguzi wa  ndani wa hesabu za Mahakama, Profesa Tolly Mbwette akitoa mada katika mafunzo hayo.

Washiriki wa  Mafunzo  wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu  Kanda ya Dodoma, Mhe. Jaji Ignas Kitus ( aliyekaa katikati ) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu-Kanda ya Dodoma, Mhe. Dynes Lyimo na kulia ni Prof. Tolly  Mbwette.
(Picha na Rashid Omar)

 
 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni