Na Jovian Katundu, Mahakama ya Wilaya Misungwi
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda
ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika amewapongeza watumishi wa Mahakama ya Wilaya
Misungwi kwa kusalia na mashauri yasiozidi miezi 3 katika Mahakama za Mwanzo na
upanuzi mdogo uliofanyika katika jengo linatumika kwa shughuli za mahakama ya
wilaya.
Mhe. Jaji Rumanyika alitoa pongezi
hizo alipofanya ziara ya ukaguzi katika Mahakama hiyo mapema
Septemba 14, ikiwa ni mara yake ya kwanza baada ya kuhamia katika Kanda hiyo.
Akisoma risala mbele ya Jaji
Mfawidhi, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Misungwi Mhe Erick Marley,
alieleza kuwa Mahakama yake imejiwekea malengo ya kuhakikisha mashauri ambayo Mahakama yake ina mamlaka nayo yasizidi miezi 6 tangu kufunguliwa kwake.
Akiongea na Watumishi wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Rumanyika amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii
na ubunifu katika kuwahudumia wateja wanaofika Mahakamani kupata huduma.
Sambamba na hayo, amewasisitiza
Watumishi wote wa Mahakama Kanda ya Mwanza kuongozwa na kauli mbiu ya Kanda
ambayo ni "Mpe raha mteja, Mahakama ing'are" kauli mbiu ambayo inampa
kipaumbele mteja ikiwa ni pamoja na kumuelimisha.
Katika ziara hiyo Mhe Jaji Mfawidhi
ameambata na Naibu Msajili Mfawidhi Kanda ya Mwanza, Mhe.Mary Moyo na Kaimu
Mtendaji wa Mahakama Kuu Bw. Ibrahimu Mohamed.
Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam Rumanyika akikaribishwa na
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya Misngwa, Mhe. Erick Marley pindi Mhe.
Jaji alipowasili katika Mahakama ya Wilaya Misungwi.
Mhe.
Jaji Mfawidhi Kanda ya Mwanza akisalimiana na Watumishi wa Mahakama hiyo mara
baada ya kuwasili.
Akisalimiana
na baadhi ya Wananchi waliokuwa wakipata huduma katika Mahakama hiyo.
Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza akisaini kitabu cha Wageni katika ofisi
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya Misungwi.
Sehemu
ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi wakimsikiliza Mhe. Jaji
Rumanyika (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam Rumanyika akiwa katika picha
ya pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Misungwi. Aliyeketi wa
kwanza kushoto ni Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Mary Moyo,
aliyeketi wa pili kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Misungwi Mhe Erick R. Marley
na wa kwanza kulia ni Afisa Utumishi, Mahakama Kuu Mwanza,Bw. Ibrahimu Mohamed.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni