Na Emmanuel
Oguda, Mahakama Kuu, Shinyanga
Viongozi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Shinyanga wamekumbushwa kutimiza wajibu wao katika kutekeleza majukumu
yao ya kuhudumia wananchi.
Akitoa maelekezo ya
utekelezaji majukumu kwa viongozi hao, mwishoni mwa wiki katika kikao cha
Menejimenti Kanda ya Shinyanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
Mahakama Kuu.Kikao hicho,kilichojumuisha viongozi wa Mahakama Mkoa wa Shinyanga
na Simiyu.
Jaji Mfawidhi
Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Mhe.Jaji Richard Malima Kibela, amesisitiza
juu ya kuzingatia taratibu, miongozo na kanuni mbalimbali zilizotolewa ili
kuhakikisha lengo la utoaji haki kwa wakati kwa wananchi linafikiwa kama ilivyo
kwenye Mpango Mkakati wa Mahakama wa Miaka mitano.
Viongozi hao ambao ni
Wahe. Naibu Wasajili, Mahakimu wakazi Wafawidhi, Watendaji wa Mahakama,
Wakaguzi wa Ndani, Afisa TEHAMA na Afisa Masjala Mahakama Kuu wamesisitizwa
kusimama katika nafasi zao kusimamia masuala ya utendaji kazi zikiwamo taarifa
mbalimbali za Mahakama, JSDS 2, Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Fedha, Miundombinu
ya Mahakama ili kuleta ufanisi na uwajibikaji kwa kila mmoja kwa nafasi yake.
Aidha, Mhe Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga alisisitiza upendo na kuthaminiana
baina ya viongozi hao na watumishi wengine kwa kuwa upendo ndio nguzo kuu ya
utendaji bora na ushirikiano huleta mafanikio makubwa katika kufikia lengo la
utoaji haki kwa wakati.
Akisisitiza juu ya
utendaji bora na utekelezaji wa majukumu,Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu
Kanda ya Shinyanga, Mhe. Sekela Mwaiseje alisema kuwa kwa sasa Mahakama hiyo
inatekeleza majukumu yake vizuri, mbali na changamoto ambazo zimekuwa
zikijitokeza lakini kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitatuliwa.
Aliongeza kwamba
wananchi wanaelimishwa kupitia kipindi cha elimu kwa wananchi ambacho hutolewa
asubuhi kabla ya kuanza Mahakama.
Mhe.Jaji Mfawidhi
alisisitiza wananchi waendelee kuelimishwa juu ya masuala mbalimbali ya
Mahakama, huku akiwataka watumishi wote kuzingatia taratibu na miongozo katika
utendaji kazi wa kila siku.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya
Shinyanga,Mhe. JaJi Richard Kibela akizungumzia kuhusu utendaji kazi kwa
viongozi wa Mahakama wa kanda hiyo.
|
Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga,Mhe. Sekela Mwaiseje akifafanua jambo. |
Wahe. Mahakimu
Wafawidhi wakimsikiliza kwa makini Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya
Shinyanga, Mhe. Kibela.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni