Na Festor Sanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kigoma
Jaji
Mfawidhi Mahakamu Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole amefanya ziara ya
kikazi kwa kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za Mahakama mkoani Kigoma
pamoja na ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Mahakama Kuu, Kanda tarajiwa
ya Kigoma.
Mhe.
Jaji Mfawidhi huyo alifanya ziara yake mkoani humo kuanzia September 17, 2018 hadi
September 21, 2018 na alipata fursa ya kukagua Mahakama katika Wilaya za wilaya
Kibondo, Kasulu, Kigoma na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma.
Akiongea na Watumishi wa Mahakama Mkoani humo hivi
karibuni, Mhe. Jaji Bongole aliwaasa kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
“Kwa
yule ambaye atatuhumiwa na kupelekwa Mahakamani na kuthibitika kushiriki katika
vitendo vya rushwa, atachukuliwa hatua stahiki za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa
kazi” alisisitiza Mhe. Jaji Bongole.
Aidha,
aliwapongeza watumishi kwa kufanya kazi
kwa ushirikiano na kuwasisitiza kuendelea kuwa na nidhamu kazini pamoja na
kufuata maadili ya utumishi wa umma ili kuboresha utendaji kazi wa shughuli za
Mahakama kwa umma.
Katika
ziara hiyo, Jaji Mfawidhi huyo alitembelea na kujionea miradi ya ujenzi wa
Mahakama ya Wilaya Kasulu na Mahakama Kuu, Kanda tarajiwa ya Kigoma
inayotarajiwa kukamilika mapema mwaka 2019.
Mbali
na ukaguzi wa Mahakama, Mhe. Bongole alipata fursa ya kutembelea Magereza ya
Wilaya ya Kasulu, Kibondo na Kigoma ili
kubaini changamoto mbalimbali zilizoko na kuzitolea ufumbuzi.
Pichani
ni muonekano wa jengo la Mahakama Kuu, Kanda tarajiwa ya Kigoma lililopo katika
ujenzi, Mhe. Jaji Mfawidhi Kanda ya Kigoma alitembelea mradi huo kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa
jengo hilo linalotarajiwa kukamilika, Juni, 2019.
Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora
(kushoto) akiongea jambo na Wakandarasi wa ‘Masasi Construction Company
Limited’ wanaojenga jengo la Mahakama Kuu tarajiwa Kigoma.
Mtendaji
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Bw. Moses Mashaka akimkaribisha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda
ya Tabora Mhe. Salvatory B. Bongole (wa pili kushoto) kabla ya kuongea na Watumishi
wa Mahakama mkoani humo (hawapo pichani). Wa pili kulia ni Naibu Msajili,
Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Beda Nyaki na wa kwanza kushoto ni Hakimu
Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Mhe. Flora Mtarania.
Mhe.
Jaji Mfawidhi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa
Mahakama ya Wilaya Kibondo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora
akipanda mti katika eneo la Mahakama ya Wilaya Kibondo ikiwa ni utekelezaji wa
azimio la kuboresha mazingira. Kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Mhe.
Fadhili Mbelwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni