Na Magreth Kinabo
Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi,Mhe. Winfrida
Korosso amewataka wadau wa jinai
wa mahakama hiyo kuharakisha upelelezi ili kesi za rushwa na uhujumu uchumi zisichukue muda
mrefu .
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji huyo, wakati
akifungua kikao cha wadau wa jinai wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, lengo la kikao hicho
ni kufanya tathimini utendaji wa
mahakama hiyo tangu ilipoanzishwa.
"Upelelezi
wa mashauri ya uhujumu
uchumi kuchukua muda mrefu, na
hivyo kusababisha mlundikano wa mashauri wa
katika Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya, ikiwa upelelezi huo
utafanyika kwa haraka kesi hizo zitasikilizwa kwa wakati,” alisema Mhe.
Korosso.
Jaji Korroso aliongeza kwamba elimu
itolewe ili kukabiliana na changamoto uelewa mdogo
wa sheria ya uhujumu uchumi kwa wadau
hasa baada ya mabadiliko yaliyopelekea kuanzishwa Divisheni . Hali hii imesababisha mashauri ya
uhujumu uchumi kuondoshwa Mahakamani kwa kutokidhi vigezo wakati wa usajili na wakati wa usikilizaji wa maombi
ya dhamana.
Aidha Mhe .Korosso.
alisema kuna umuhimu wa elimu kutolewa
kuhusu Sheria ya Udhibiti wa Madawa ya kulevya baada ya kufanyiwa marekebisho
mwaka 2017. Marekebisho yaliyofanyika yameathili vifungu vingi vya sheria
hiyo.
Mhe. Korosso
aliomba ushirikiano kutoka kwa wadau wa
mahakama hiyo ili kuiwezesha kutimiza majukumu yake kwa wakati.Pia alizitaka
taasisi nyingine kuwezeshwa kirasilimali watu na fedha.
Akizungumzia kuhusu utendaji kazi wa mahakama hiyo,
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu –Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Charles
Magesa alisema
imesajili kesi za maombi ya dhamana 311 nchi nzima tangu
Julai 2017 hadi sasa na wamesikiliza 270 na zimeshatolewa maamuzi.
Kwa upande wa
Uhujumu uchumi kesi zilizosajiliwa ni
29, kati ya hizo zilizomalizika ni saba na 22 bado zinaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni