Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwasili katika kisiwa cha Ukerewe kuanza ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama katika Mkoa wa Mwanza. Leo Jaji Mkuu alitembelea Mahakama ya wilaya ya Nansio- Ukerewe, Mahakama za Mwanzo za Nansio mjini na Ilangala pamoja na Ofisi ya Mkuu wa wilaya. Katikati ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Mary Moyo.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama baada ya kumkabidhi kitabu cha Mpango huo Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya (DAS) Bwana Focus Majumbi wakati Jaji Mkuu alipotembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nansio-Ukerewe wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi hao katika ziara yake katika mkoa wa Mwanza. Aidha, Jaji Mkuu aliwataka watumishi hao kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha mashauri yanamalizika kwa wakati.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nansio mara baada ya kuzungumza nao.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ilangala mara baada ya kuzungumza nao.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Mkewe mama Anna Abdalah alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Mkewe mama Anna Abdalah alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe. Wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania.
JAJI
MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI
Na
Lydia Churi- Mahakama, MwanzaJaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka watumishi wa Mahakama katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza hususan Mahakimu kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa kuhakikisha wanamaliza kesi ili wananchi waweze kupata haki kwa wakati.
Akizungumza na
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nansio-Ukerewe pamoja na Mahakama za Mwanzo
za Ilangala na Nansio mjini, Jaji Mkuu pia amewakumbusha Mahakimu kuhakikisha hukumu
zinatolewa ndani ya siku 90 baada ya shauri kusikilizwa na endapo siku zitazidi
basi zisizidi siku ishirini na moja.
Alisema Mahakama ya
Tanzania inafanya kila jitihada ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa
wakati huku akitolea mfano wa nakala za hukumu kutolewa bure. Alisema Mahakama
imeingia mkataba na shirika la Posta ili kusambaza nakala za hukumu pamoja na
nyaraka nyingine za mahakama.
“Suala la hakimu kuchelewesha
hukumu bila sababu za msingi halikubaliki na ni utovu wa nidhamu, jiwekeni
kwenye nafasi ya wanaocheleweshewa hukumu ndipo mtaona ni kwa namna gani
wanaumizwa na suala hili”, alisema Jaji Mkuu.
Awali akizungumza na
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukererwe Bwana Focus Majumbi, Jaji Mkuu alitoa wito kwa
viongozi wa serikali kusaidia kuwaelimisha wananchi taratibu za Mahakama ili wapate
haki kwa wakati kwa kuwa haki ni kwa mujibu wa Sheria.
Alisema wananchi wengi
hawafahamu taratibu za Mahakama ambapo badala ya kudai haki zao Mahakamani huenda
kwa watu wasiohusika na kusababisha haki zao kuchelewa.
Naye Kaimu Mkuu wa
wilaya ya Ukerewe aliiomba Mahakama ya Tanzania kuanza kuitumia Mahakama ya
Mwanzo ya Irugwa ambayo hivi sasa haijaanza kutumika kutokana na ukosefu watumishi. Mkuu huyo wa wilaya pia aliiomba
Mahakama kusaidia ili wilaya yake isaidiwe kupata Mwenyekiti wa kudumu wa
mabaraza ya kata.
Jaji Mkuu wa Tanzania anaendelea
na ziara yake ya siku nne mkoani Mwanza ambapo atakagua utekelezaji wa shughuli
za Mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni