Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
(kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella,
Mhe. Jaji Mkuu alipata wasaa wa kutoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na
wananchi wote waliopatwa na maafa ya kivuko cha MV Nyerere yaliyotokea
Septemba, 20, 2018 katika wilaya ya Ukerewe.
Aidha;
Mhe. Jaji Mkuu alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano katika ya ofisi yake na
Mahakama mkoani humo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella nakala ya kijitabu cha
Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama ya Tanzania, pindi Mhe. Jaji
Mkuu alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo, wa pili kushoto ni Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Sam Rumanyika.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.
John Mongella (wa nne kushoto), Mhe. Jaji Mkuu aliyetembelea
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita aliambatana na Jaji Mfawidhi,
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Jaji Sam Rumanyika (wa tatu kulia) na baadhi ya Maafisa wa
Mahakama mkoani Mwanza.
(Picha kwa hisani ya Ibrahimu Mohamedi, Mahakama Kuu
Mwanza)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni