Na Victor Kitauka, Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro
Mahakama ya Tanzania haiwezi
kutekeleza Mpango Mkakati wake bila kushirikisha na kushauriana na Wadau wake
katika jukumu la utoaji haki kwa wananchi.
Hayo yalisemwa Oktoba 11 na Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mh. Dr. Eliezer M. Feleshi alipokuwa akifungua
Mkutano wa Mashauriano kati ya Mahakama ya Tanzania na Madalali wa Mahakama na
Wasambaza Nyaraka mjini Morogoro katika hotel ya Morogoro Hotel.
Mhe. Jaji Kiongozi alisema
kuwa Mkutano huo ni muhimu sana kwa Mahakama na kwa Wadau (Madalali
wa mahakama na Wasambaza Nyaraka ambao ni maafisa wa Mahakama) waliohudhuria
katika Mkutano huo.
“Mkutano huu ni wa kihistoria kwa
sababu ni Mkutano unaofanyika kwa mara ya kwanza na pia umewaleta pamoja
Madalali na Wasambaza Nyaraka za Mahakama ambao wamehudhuria mafunzo na
kufaulu usaili wa kuomba kazi ya Udalali na Usambazaji Nyaraka,” alieleza Mhe.
Jaji Kiongozi.
Akizungumzia mkutano huo, Mhe. Jaji
Kiongozi alisema lengo ni kujadili na kutathmini masuala mbalimbali yanayohusiana
na kazi/huduma wanazofanya Madalali na Wasambaza Nyaraka kwa wadau
wengine wa Mahakama.
Kupitia mkutano huu wanatarajia kuja
na maazimio ambayo yatasaidia sana katika kutekeleza majukumu ya Mahakama
ambayo lengo kuu ni kuiwezesha mahakama kutoa haki kwa wakati.
pia ni mara ya kwanza tangu wameingia kwenye
jukumu hilo kwa muundo na sasa na miongozo wa sasa unaosimamia utendaji wa kazi
za madalali na Wasambaza Nyaraka kukutana.
Mahakama ya Tanzania kupitia mpango
mkakati wake wa mwaka 2015/2020 ambao una nguzo tatu, ya kwanza ikiwa ni
utawala na uwezeshaji, ya pili ni kuhimili kazi kuu ya utoaji haki na tatu ni
kuifanya kazi ya mahakama iaminike na kujenga misingi imara ya
kushirikia na na wadau wake, na kupitia nguzo ya tatu ndio sababu ya mkutano
huu, kwani mahakama umeona haiwezi kufanya majukumu yake bila kupata
ushirikiano wa dhati, mipango ya pamoja na hata kushauriana na wadau
wake.
Akielezea umuhimu wa Wadau hao katika utoaji wa haki, Mhe. Jaji alisema kuwa wana jukumu kubwa la kutekeleza na kuwezesha
usikilizwaji wa mashauri kwa maana ya usambazaji wa nyaraka lakini
kutekeleza ukazaji wa hukumu kwa kufika tamati ya wadaawa na hivyo kuwezesha
haki kupatikana kwa wakati.
hivyo kutenda vizuri kwa muhusika mmoja
au sehemu moja ndani ya mkondo wa utoaji haki hakuwezi kukafanikiwa kama upande
au muhusika mwingine hawezi akashikamana na hilo na ndio sababu mahakama
ikaona kujenga uwezo wa madali na Wasambaza Nyaraka ni jambo la msingi katika
kutekeleza majukumu yake.
Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwakumbusha
Wadau hao juu ya umuhimu wa kuanzisha chama chao ili kiweze kuwa kama daraja la
mawasiliano na Mahakama na pia katika kuwasilisha mapendekezo ya kuboresha kazi
zao, changamoto mbalimbali.
“Vilevile Chama kitasaidia kudhibiti
Madalali na Wasambaza Nyaraka wanaokwenda kinyume na miiko ya
udalali ili kulinda hadhi na heshima ya madalali na Wasambaza Nyaraka,”
alisisitiza. Mhe. Jaji Dkt. Feleshi.
Mkutano huo wa siku mbili (2) uliudhuliwa
pia na Mwakilishi kutoka katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Polisi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wengine ni Wawakilishi kutoka TRA,
BRELA, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Manaibu Wasajili wa Mahakama
Kuu na Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Mahakama ya Tanzania na Madalali wa Mahakama na
Wasambaza Nyaraka uliofanyika katika hoteli ya Morogoro mkoani Morogoro.
Sehemu ya
Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kinachojiri.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi wa tatu kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na Washiriki wa Mkutano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni