Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi
Lindi, Mhe.James Karayemaha (aliyeketi mbele kushoto), akizungumza na Watumishi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi mwishoni mwa wiki kuhusu masuala mbalimbali yenye kuleta Ufanisi wa Utoaji
Haki kwa wakati pamoja na tathmini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama
ya Tanzania wa Mwaka 2015/2016-2019/2020 kwa Mahakama hiyo.
Mtendaji
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Bw. Joseph
Chota (aliyeketi mbele kulia) akizungumza na Watumishi wa Mahakama hiyo,
miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na Mfumo wa
kusajili mashauri kwa njia ya Kieletroniki ujulikanao kama JSDS II na
Changamoto za Mfumo huo.
Lengo
la kikao hicho ni kujadili masuala mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma ya
utoaji haki.
(Picha
Hillary Rory, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Lindi)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni