Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
amewakumbusha Majaji na Mahakimu kutumia
Mamlaka waliyonayo kisheria kutoa adhabu zinazoirekebisha jamii kwa makosa
yanayojirudia mara kwa mara.
Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
ya Kwimba leo Jaji Mkuu alisema Mahakama ni sehemu ya jamii hivyo inalo jukumu
la kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani na salama.
Kuhusu ushirikiano kati ya Mahakama na mihimili mingine,
Jaji Mkuu alisema katiba ya nchi imegawanya majukumu kwa kila mhimili lakini yote
inaunganishwa na dhana moja ya
kuwatumikia wananchi, hivyo aliahidi kuendeleza ushirikiano na wadau wote ili wananchi
wapate haki kwa wakati.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama haiwezi kufanya
kazi peke yake bila kushirikiana na mihimili mingine. “Nguvu ya Mahakama
inatokana na nguvu kutoka kwenye mihimili mingine”, alisema.
Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake, Mkuu wa
wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga
alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mimba za utotoni hasa kwa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao hulazimika kukatisha masomo
yao.
Kuhusu ushirikiano na Mahakama, Mkuu huyo wa wilaya
alisema ofisi yake inashirikiana kwa karibu na Mahakama katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazojitokeza ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa
amani.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake katika mkoa wa
Mwanza ambapo anakagua shughuli za Mahakama. Tayari ameshatembelea baadhi ya
Mahakama zilizopo kwenye wilaya za
Ukerewe, Sengerema na Kwimba.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kwimba baada ya kuzungumza nao leo katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za kimahakama wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Happyness Ndesamburo.
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania (hayupo pichani)
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na viongozi wengine wa Mahakama na Mahakimu wa Mahakama zilizopo wilayani Kwimba mara baada ya kuzungumza nao.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na viongozi wengine wa Mahakama na watumishi wa Mahakama zilizopo wilayani Kwimba mara baada ya kuzungumza nao.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga pamoja na Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Mansoor Shanif Hiran.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni