Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (wa tatu kulia) pamoja na baadhi ya
Wahe. Majaji wengine wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika
hafla ya kuwaaga rasmi Wahe. Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu.
Pichani ni Jaji Mstaafu
wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Augustine Shangwa mmoja kati ya
Wahe. Majaji Wastaafu walioagwa rasmi kitaaluma katika Ukumbi namba. 2 wa
Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Laurence Kaduri (katikati) akitoa
neno la shukrani katika hafla ya kuwaaga rasmi kitaaluma, iliyofanyika Oktoba
26, Mahakama Kuu Dar es Salaam.
Pichani ni Jaji Mstaafu
wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Aloysious Mujulizi akitoa neno
katika hafla hiyo, Mhe. Jaji Mujulizi ameishauri Mahakama kuangalia uwezekano
wa matumizi ya lugha la Kiswahili katika usikilizaji na uendeshaji wa kesi kwa
ujumla.
Miongoni mwa wageni
waalikwa na Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika hafla ya kuwaaga rasmi
Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi akitoa neno la pongezi kwa Wahe.
Majaji Wastaafu, pongezi hizo alitoa kwa niaba ya Mhe. Jaji Kiongozi na Majaji wa Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Naibu Msajili
Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba akitoa mwongozo wa hafla
ya Kuwaaga rasmi Wahe. Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
kushoto ni Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.
Joachim Tiganga.
Jaji Kiongozi-Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (wa tatu kushoto) pamoja na baadhi
ya Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya
pamoja na Wahe. Majaji Wastaafu walioagwa rasmi kitaaluma. Wahe. Majaji
walioagwa ni pamoja na Mhe. Augustine Shangwa (wa pili kushoto), Mhe. Laurence
Kaduri (wa tatu kulia), Mhe. Aloysious Mujulizi (wa kwanza kushoto) wengine
walioagwa Kitaaluma ambao hawapo pichani ni Mhe. Mwaikugile, Mhe. Sheikh, Mhe.
Mwakipesile na Mhe.Jaji Malecela.
Picha ya pamoja kati ya
Mhe. Jaji Kiongozi, Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Wahe.
Majaji Wastaafu pamoja na Sehemu ya Manaibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama-
Dar es Salaam.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni