Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo wa Mahakama ya Tanzania Mhandisi
Khamadu Kitunzi (kulia) akimuelezea jambo Msimamizi wa Mradi huo Bwn. Hussein Majaliwa (kushoto) wakati alipokwenda mkoani Katavi kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi na Mahakama ya wilaya ya Mpanda. Mhandisi Kitunzi alimtaka Msimamizi huyo kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo linalotakiwa kukamilika kabla ya mwezi Julai, 2019.
Mhandisi Khamadu Kitunzi akisitiza jambo kwa Msimamizi
wa mradi huo Bw. Majaliwa Hussein. Aliyesimama (Kushoto) ni Afisa tawala wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi Bw. Nicas Msangi.
Katika picha ni hatua
ya sasa ya ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi – Katavi na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda zitakazokuwa katika jengo
moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni