Jumatatu, 29 Oktoba 2018

MHE. JAJI MSTAAFU CHOCHA AAGWA KITAALUMA-MBEYA


Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Noel  Chocha (aliyeketi upande wa juu wa pili kulia) ameagwa rasmi kitaaluma mapema  Oktoba, 26,  2018 katika ukumbi Namba 4 wa wazi wa Mahakama katika jengo la Kituo Jumuishi. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Watumishi wa Mahakama, Majaji wa Mahakama Kuu ambao ni Mhe. Robert Makaramba (katikati), Mhe. Dkt. Mary C. Levira (wa kwanza kushoto), Mhe. Dkt. Benhaj Masoud (wa pili kulia)na Mhe. Paul J. Ngwembe, wadau muhimu wa Mahakama pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila aliyeambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya. Aliyeketi mbele ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. George Hurbert.

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Mbeya Mhe. Noel Chocha (katikati) akizungumza na wageni waliohudhuria. Katika hotuba yake amewataka wadau wote wa haki kuendelea kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuwahudumia wananchi ipasavyo. 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila (katikati) akifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa. 

Kaimu Wakili wa Serikali Mfawidhi, Mhe. Catherine Gwaltu akisoma hotuba kwa niaba ya Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali. Katika hotuba hiyo alimpambanua  Mhe. Jaji Chocha kama Jaji aliyekuwa mzalendo, mtetezi wa haki na Jaji aliyekuwa akifanya maamuzi kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Mkoani Mbeya, Mhe. Joyce Kasebwa akitoa neno katika sherehe hiyo.


Jaji Mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Noel Chocha (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama. Wa tatu kushoto ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba, wa pili kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Mhe. Dkt. Mary Levira, wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Dkt. Benhaj Masoudna wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu katika Kanda hiyo, Mhe. Paul Ngwembe.

(Picha na Rajab Singana, Mahakama Kuu, Mbeya)
 
 
 




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni