Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi
ya Majaji wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kuwaaga Majaji
Wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kulia ni mmoja wa Majaji Wastaafu wa
Mahakama Kuu, Mhe. Regina Rweyemamu, Majaji wengine waliostaafu kwa mujibu wa
Sheria ni Mhe. Jaji Frederick Werema na Mhe. Jaji Ibrahim Mipawa.
Pichani ni Jaji Mstaafu
wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Biashara, Mhe. Jaji Frederick Werema akiwa katika
hafla ya kuagwa kwao Kitaaluma katika Ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya
Tanzania-Dar es Salaam mapema Novemba 30, 2018. Wahe. Majaji Wastaafu kwa
ujumla wao wameishukuru Mahakama kwa kushirikiana nao vyema katika kipindi cha
utumishi wao na vilevile kuwaasa Watumishi wa Mahakama waliopo kazini
kujiepusha na Vitendo vya Rushwa.
Baadhi ya Wageni
waalikwa na Watumishi wa Mahakama wakiwa katika hafla ya kuagwa rasmi Kitaaluma
Majaji watatu Wastaafu wa Mahakama Kuu.
Mwakilishi kutoka Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akisoma Wasifu wa Wahe. Majaji Wastaafu katika
hafla hiyo.
Mtendaji wa Mahakama
Kuu, Bw. Leonard Magacha (mwenye suti nyeusi) pamoja na Watendaji wengine wa
Mahakama na baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakiwa katika hafla hiyo.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi (katikati), baadhi ya Majaji wa
Mahakama Kuu na sehemu ya Watumishi wa
Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji Wastaafu wa Mahakama
Kuu, wa tatu kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Jaji Frederick Werema, wa tatu kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Jaji
Regina Rweyemamu, wa pili kulia ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi,
Mhe. Jaji Aisha Nyerere, wa kwanza kulia ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Beatrice Mutungi na wa kwanza kushoto ni Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu-Divisheni ya Biashara, Mhe.Jaji Barke Sehel.
Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu-Divisheni ya Biashara, Mhe.Jaji Barke Sehel (kushoto) akimpatia shada la
maua Jaji Msataafu, Mhe. Frederick Werema aliyesimama na Mhe. Werema ni mkewe.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi (kushoto)akimpongeza Jaji
Mstaafu, Mhe. Jaji Regina Rweyemamu kwa shada la maua, kulia ni Jaji Mfawidhi,
Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi, Mhe. Jaji Aisha Nyerere.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi (kushoto) akimpongeza Jaji
Mstaafu, Mhe. Ibrahim Mipawa (kushoto), kulia ni Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu-Divisheni ya Kazi, Mhe. Jaji Aisha Nyerere.
Picha ya pamoja na
ndugu wa Mhe.Jaji Mstaafu, Mhe. Regina Rweyemamu
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni