Na mwandishi wetu
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe, Profesa Ibrahim Juma
amesema Mahakama ya Tanzania iko tayari kushiki na Taasisi ya Urudishaji
wa Mali zilizotoroshwa na Utakatishaji wa Fedha (ARINSA).
Akizungumza na ujumbe wa watu watano kutoka
nchi mbalimbali, ukiongozwa na Mshauri,Fitz -Roy Drayton Jaji Mkuu alisema Mahakama iko tayari kushiriki na taasisi
hiyo katika mafunzo ili kupata uzoefu
kutoka nje katika maeneo hayo.
Aidha Jaji
Mkuu aliwashukuru wageni hao kwa kazi kubwa wanazozifanya katika nchi hizo,
kwani ni muhimu kwa sasa kukuza uchumi ambao keki
ya mataifa haya iwe kwa manufaa
ya watu wote na sio kwa wajanja wachache.
Hivyo
utekelezaji wa sheria hizi ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi wenyewe.
Jaji Mkuu
alimwelezea Msajili wa Mahakama ya Rufani (RCA), Mhe. John Kahyoza
kuangalia namna bora katika kalenda
ya Mahakama ili ARINSA iweze kutoa mafunzo kwa majaji na mahakimu.
Awali akizungumzia kuhusu ujio wa wageni hao,
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) Biswalo Mganga alisema kazi yao kubwa kushirikisha nchi za Kusini mwa Afrika katika
kuhusu sheria za kila nchi katika kurudisha mali zilitoroshwa, kuchukua au
kufilisi fedha zilizotakaswa.
Naye Mshauri
wa ARINSA, Fitz -Roy Drayton
alisema kazi nyingine watatoa
taarifa ripoti za sheria kuonyesha mataifa yanayofanyakazi katika eneo
hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni