Jumanne, 6 Novemba 2018

MAAFISA HABARI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WATEMBELEA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA KUHABARISHA UMMA

 Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika chumba cha Habatri cha gazeti la HabariLeo walipotembelea Ofisi za Shirika la Magazeti ya Serikali kwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuuhabarisha Umma. Wa pili kushoto ni Kaimu Mhariri wa gazeti la Habari Leo Bwana Nicodemus Ikonko na wa pili kulia ni Mtaalamu Mwelekezi wa Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Dkt. Cosmas Mwaisobwa, Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe. Wa kwanza kulia ni Afisa Habari Mwandamizi, Lydia Churi na wa kwanza kushoto ni Afisa Habari, Mary Gwera.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wa gazeti la Habari leo na SpotiLeo wakiwa katika chumba chao cha Habari.
 Mhariri wa Makala wa gazeti la HabariLeo Bw. Nelson Goima (kushoto) akiwaelezea Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania kuhusu utendaji kazi wa gazeti la Habari Leo kwa upande wa uandishi wa Makala. 
 Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mtaalamu Mwelekezi wakifuatilia jambo wakati wa ziara yao katika Shirika la Magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers) leo 
jijini Dar es salaam.
 Mtaalamu Mwelekezi wa Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Dkt. Cosmas Mwaisobwa akimwelezea jambo Mwandishi wa Habari Mwandamizi Rodgers Luhwago katika chumba cha Habari cha gazeti la Daily News.
 Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania pamoja na wenyeji wao wakizungumza na waandishi wa Habari wa gazeti la Daily News (hawapo pichani)  walipokuwa katika chumba cha Habari cha gazeti hilo.

 Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe akimkabidhi nakala za vitabu vinavyoelezea Mpango Mkakati wa miaka Mitano wa Mahakama, Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Bibi. Tuma Abdallah wakati wa ziara ya Maafisa Habari wa Mahakama katika shirika hilo.
 Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Bibi. Tuma Abdalah akimkabidhi Fulana Maalum za Shirika hilo Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe. Pamoja na kutoa zawadi hiyo, Naibu Mhariri Mtendaji pia aliahidi kushirikiana kwa karibu na Mahakama ya Tanzania katika masuala yote yanayohusu kuuhabarisha Umma.  

 Mhandisi Mwandamizi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Shirika la Magazeti ya Serikali, David Celestine akiwaelezea jambo Maafisa Habari wa Mahakama walipotembelea katika eneo lake.  

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe akiwaelezea Waandishi wa Habari wa gazeti la Daily News (hawapo pichani) kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa maboresho ya huduma za mahakama jambo katika chumba cha Habari cha gazeti la Daily News.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni