Na Paul Mushi, Mahakama Kuu-Moshi
Mahakama Kuu, Kanda
ya Moshi imemuaga rasmi Kitaaluma aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu katika
Kanda hiyo, Mhe. Jaji Mstaafu Aishiel Sumari.
Sherehe za
kumuaga kitaaluma zilizohudhuriwa na Wahe. Majaji na Watumishi wa Kanda hiyo pamoja
na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Mkoa na Mawakili zilifanyika Novemba
06, katika eneo la Mahakama Kuu Kanda ya
Moshi ikiwa ni hitimisho la safari yake katika Utumishi wa Umma.
Katika hotuba
yake Mhe. Jaji Mstaafu Sumari aliwashukuru Viongozi wa Mahakama ya Tanzania na Watumishi
wote wa Mahakama kwa ujumla kwa kushirikiana nae katika kipindi chote cha
utumishi wake.
“Kwa namna ya
pekee napenda kuwashukuru pia watumishi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza niliofanya
nao kazi kuanzia 2006 hadi Dec 2014 na Mahakama Kuu Kanda ya Moshi January 2015
hadi Nov 2018,” alisema Mhe. Jaji Mstaafu Sumari.
Katika Utumishi
wa Umma, Mhe. Jaji Mstaafu Sumari aliwahi kushika nafasi mbalimbali mfano
katika Ofisi ya Mwanasheria kuanzia mwaka 1984 hadi 2003 kama Mwanasheria wa
Serikali.
Mwaka 2003
alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Makosa ya Jinai, Rushwa na Uhujumu
Uchumi.
Mwaka 2006, Rais Mstaafu wa Serikali wa awamu wa nne, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Mhe. Aishiel Sumari kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania.
Mhe. Jaji Mstaafu
Sumari amelitumikia Taifa kwa muda wa miaka 34 hadi kufikia leo tarehe
06/11/2018 alipohitimisha safari ya Utumishi wa Umma.
Kwa Mujibu wa
taratibu za Kimahakama Jaji anapostaafu hustaafishwa kwa kufanyika shauri
maalumu ambalo ndilo hasa huitimisha zoezi zima la kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, ambaye pia alikuwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. Aishiel Sumari (wa nne kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu na Mawakili walioshiriki katika hafla ya kumuaga kitaaluma iliyofanyika Novemba 06, 2018.
Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Mhe. Aishiel Sumari (wa nne kushoto)
akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya
Moshi na Arusha, Majaji Wastaafu pamoja na sehemu ya Watumishi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Moshi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni