Uongozi
wa kampuni ya saruji Tanga (Simba cement) umekabidhi jezi za mpira wa pete (20)
na miguu (22) kwa uongozi wa Mahakama Kanda ya Tanga ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
yao waliyoitoa walipopelekewa ombi maombi hayo.
Akikabidhi
jezi hizo mwisho wa wiki, Mwanasheria wa Simba Cement Ndugu. Deogratias Mhagama, ameushukuru
Uongozi wa Mahakama kwa kuwashirikisha katika kufanikisha michezo ndani ya
Mahakama ikiwa ni kielelezo cha Mahakama kuwa ni sehemu ya jamii.
Akipokea
jezi hizo Jaji Mfawidhi Mhe. Amiri Mruma, ameushukuru uongozi wa Simba Cement
na kuwahakikishia kwamba, jezi hizo zitakuwa kichocheo cha kuhamasisha na
kuimarisha Timu ya Mahakama ili iweze kuwa mshindani kwenye Mabonanza na
michezo mbalimbali itakayoshiriki ndani nan je ya Kanda.
Aidha Jaji Mruma
ameupongeza Uongozi wa Simba Cement kwa
moyo wao wa uzalendo na kimichezo waliouonesha kupitia ufadhili huo ambao pia
unaiweka Mahakama karibu na Wananchi.
Mwanasheria
wa Simba Cement, Bw. Deogratias Mhagama (kushoto) akimkabidhi jezi, Jaji
Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Mruma (kulia).
Jaji
Mruma akiongea na uongozi wa Mahakama pamoja na wawakilishi wa Simba Cement.
Uongozi
wa Mahakama, Wajumbe wa Kamati ya Michezo wa Mahakama pamoja na wawakilishi wa
Simba Cement waliohudhuria kwenye tukio la kukabidhi Jezi.
(Picha
na Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni