Jumanne, 13 Novemba 2018

ZINGATIENI MAADILI MNAPOTOA HUDUMA KWENYE MAHAKAMA INAYOTEMBEA


Na Lydia Churi-Mahakama
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati amewataka watumishi wa Mahakama hususan watakaotoa huduma kwenye magari maalum yatakayokuwa yakitoa huduma za Mahakama (Mahakama inayotembea) kufanya kazi hiyo kwa weledi, ubunifu, kufuata sheria za nchi na kuzingatia maadili ili wananchi wapatiwe huduma bora.

Akifunga Mafunzo ya siku mbili kwa watumishi wanaotarajiwa kutoa huduma kwenye Mahakama inayotembea, Msajili Mkuu amewataka watumishi hao kukataa vitendo vya rushwa, na kutotumia lugha isiyofaa wanapowahudumia wananchi wanaofika Mahakamani kutafuta haki zao.

Alisema kwa kufanya hivyo, watumishi hao wataiwezesha Mahakama ya Tanzania kufikia malengo yake ya kutoa huduma bora na kuwapatia wananchi haki kwa wakati.
“Nitasikitika sana endapo nitasikia kuwa mnatoa huduma kwa wananchi huku mkitumia lugha isiyofaa, au mkijihusisha na vitendo vya rushwa na vitendo vingine  vyovyote visivyofaa”, alisema Mhe. Revocati.

Aidha, Msajili Mkuu pia aliwataka watumishi hao kutumia mafunzo waliyoyapata ili kubadili mitazamo yao katika kutoa huduma kwa kuwapenda wateja hata kama wateja hao watawaudhi wakati wakiwahudumia.

Kurugenzi ya Menejimenti ya Mashauri ya Mahakama ya Tanzania iliandaa mafunzo ya siku mbili kwa watumishi wa Mahakama watakaokuwa wakitoa huduma kwenye Mahakama inayotembea pindi huduma hiyo itakapoanza hivi karibuni. Mafunzo hayo yaliandaliwa ili kuwajengea uwezo watumishi hao.

Mahakama ya Tanzania inakusudia kutumia magari maalum kuendeshea shughuli za Mahakama ili kumaliza mashauri kwa wakakti na kupunguza mlundikano wa mashauri.

Magari hayo yanatarajiwa kutoa huduma hiyo katika majiji ya Dar es salaam na Mwanza ambapo katika jiji la Dar es salaam huduma hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa katika maeneo ya Chanika (Ilala), Buza (Temeke), Kibamba (Ubungo) na Bunju (Kinondoni).
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akifunga mafunzo ya siku mbili ya Watumishi wa Mahakama watakaotoa huduma kwenye magari maalum yatakayokuwa yakitumika kufanya shughuli za Mahakama (Mahakama inayotembea) yanayotarajiwa kuanza kufanya kazi hiyo hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya na kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
 Mhe. Joachim Tiganga 


  Baadhi ya Watumishi wa Mahakama wakiwemo Mahakimu, Makarani na Makatibu Mahususi wakimsikiliza Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akifunga mafunzo hayo. 


   Baadhi ya Watumishi wa Mahakama  wakimsikiliza Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akifunga mafunzo hayo. 


  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu mara baada ya kufunga mafunzo ya siku mbili ya Watumishi wa Mahakama watakaotoa huduma kwenye magari maalum yatakayokuwa yakitumika kufanya shughuli za Mahakama (Mahakama inayotembea) Wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam Bwn. Gasto Kanyairita.


  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makarani na Makatibu Mahususi mara baada ya kufunga mafunzo ya siku mbili ya Watumishi wa Mahakama watakaotoa huduma kwenye magari maalum yatakayokuwa yakitumika kufanya shughuli za Mahakama (Mahakama inayotembea) 


 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania mara baada ya kufunga mafunzo ya siku mbili ya Watumishi wa Mahakama watakaotoa huduma kwenye magari maalum yatakayokuwa yakitumika kufanya shughuli za Mahakama (Mahakama inayotembea). 
Magari maalum yatakayokuwa yakitumika kufanya shughuli za Mahakama (Mahakama inayotembea) kama yanavyoonekana pichani. 
Gari maalum litakalotumika kutoa huduma za kimahakama (Mahakama inayotembea) kama linavyoonekana pichani. 
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akiwa ndani ya gari maalum litakalotumika kutoa huduma za kimahakama 
 Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa nje ya magari yatakayotoa huduma za Mahakama walipotembelea ofisi ya Toyota kuyaona magari hayo. 
 Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo ya namna ya kutoa huduma kwenye magari malum yatakayotumika kusikiliza mashauri. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni