Jumatano, 12 Desemba 2018

JAJI MKUU AMALIZA ZIARA MKOANI DODOMA

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kongwa alipofika ofisini kwa Mkuu wa wilaya hiyo kumtembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mahakama za mkoa wa Dodoma aliyoimaliza jana. Lengo la ziara hiyo ni kutathimini hali ya utoaji wa haki na kukagua shughuli za Mahakama. 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai akizungumza wakati wa ziara ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa. Kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya ya Kongwa pamoja na ujumbe wa Jaji Mkuu kutoka Mahakama ya Tanzania walioambatana naye kwenye ziara . Wa nne kulia ni Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na wa tatu kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati. Wa nne kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Jabir Shekimweri na wa tatu kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma
Mhe. Ignas Kitusi.  
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimkabidhi Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Jabir Shekimweri kitabu kinachoelezea Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania. 

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kongwa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai .
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kongwa mara baada ya kuzumza nao.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kongwa (hawapo pichani).
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kongwa wakimsikiliza Jaji Mkuu alipozungumza nao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni