TANZIA
Mahakama ya Tanzania
inasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Stephen
Ernest Ihema kilichotokea tarehe 11/12/2018 katika hospitali ya Hindu Mandal jijini
Dar es salaam.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu MbweniJKT/Ndege
Beach na Mazishi yatafanyika kesho Jumamosi Tarehe 15/12/2018 saa 10
jioni katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Marehemu Jaji Mstaafu Ihema alizaliwa mwaka1943
mkoani Shinyanga. Aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania kama Hakimu tarehe 6 May, 1969.
Aidha, Marehemu Ihema aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria
(The Law Reform Commission of Tanzania) ambapo alifanya kazi mpaka alipostaafu kwa
mujibu wa sharia tarehe 30 Juni, 1998.
Aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 3 Machi mwaka 1999. Aidha,
tarehe 1 mwezi Julai mwaka 2003 alistaafu rasmi wadhifa wa Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania.
Mwezi Julai 18, mwaka 2005, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alimteua Marehemu Jaji Ihema kuwa Kamishna wa Secretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma wadhifa ambao alikaa nao mpaka mwaka
2010.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni