Msajili Mkuu, Mahakama
ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (aliyesimama) akizungumza na Wageni kutoka
Chama cha Wanasheria cha nchini China (CLS) wakati ujumbe huo ulipotembelea ofisini
kwake kwa lengo la kujua mfumo mzima wa utendaji kazi wa Mahakama, vilevile kuwa na ushirikiano wa pamoja katika masuala ya Kisheria, aliyeketi
katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Mhe. Jaji Dkt. Benhajj Shaaban Masoud ambaye alimuwakilisha Mhe. Jaji Kiongozi
katika mazungumzo hayo, kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto (IJA), Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu
wa Chama cha Wanasheria China, Bw. Wang Wei ambaye pia ni Kiongozi wa msafara huo
akiwatambulisha Wajumbe alioambatana nao, aidha Bw. Wei alitumia fursa hiyo pia
kuikaribisha Mahakama ya Tanzania kushiriki katika Semina na Makongamano
mbalimbali yanayotarajia kufanyika nchini humo, mwaka huu.
Sehemu ya Wageni hao
kutoka Chama cha Wanasheria cha China wakiwa katika Mazungumzo.
Naibu Msajili
Mwandamizi, Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Elizabeth Mkwizu akiwa pamoja na
Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya katika mazungumzo hayo.
Mkuu
wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania (JDU), Mhe. Zahra Maruma
akiwasilisha kwa wageni hao kuhusu maboresho mbalimbali na Mikakati iliyopo
chini ya Mradi wa Maboresho wa huduma za Mahakama.
Msajili Mkuu Mahakama
ya Tanzania akimkabidhi zawadi za nakala za vijitabu vya Mpango Mkakati wa
Mahakama pamoja na Majarida ya Mahakama kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria China,
Bw. Wang Wei.
Msajili Mkuu, Mahakama
ya Tanzania (kulia) akifurahia zawadi kutoka kwa Naibu Mkururgenzi Mkuu wa CLS,
Bw. Wang Wei.
Mhe. Revocatti
akiwaonesha wageni hao Ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar
es Salaam.
(Picha na Mary Gwera,
Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni