Na Magreth Kinabo
Waziri wa Katiba na Sheria,
Palamagamba leo amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Taasisi ya Slynn kutoka
nchini Uingereza.
Mazungumzo hayo yamefanya katika ofisi ya Mahakama Kuu
jiji Dar es Salaam, ambapo Waziri huyo
aliyataja maeneo ambayo yanahitaji ushirikiano wa mafunzo
mbalimbali, yakiwemo ya makosa ya jinai.
“Tunahitaji
ushirikiano katika kuwajengea uwezo majaji na kubadilishana uzoefu,
ikiwemo kubadilishana uzoefu katika masuala ya kesi za jinai hususan zile zenye makosa
makubwa na zenye changamoto,” alisema
Profesa Kabudi.
Profesa Kabudi aliongeza kwamba mafunzo mengine ni katika maadili na ujuzi
mbalimbali wa kisheria..
Lengo la ujumbe
huo, kutembelea Mahakama ya Tanzania ni pamoja na kujua taratibu mbalimbali za
uendeshaji mashauri, kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi na vilevile
kuona jinsi gani Taasisi inasaidia katika maeneo yatakayobainishwa,” alisema
Bi. Fenney.
Taasisi ya Slynn iliyopo nchini Uingereza ina takribani
umri wa miaka 30 inajihusisha na masuala ya haki na sheria na inafanya
kazi kwa karibu na Majaji na Taasisi za
haki duniani ili kuboresha mifumo ya utoaji haki na uongozi wenye kufuata
misingi ya sheria.
Ujumbe huo ambao umefanya
ziara ndani ya Mahakama kwa siku nne umejielekeza kujua zaidi jinsi gani
Mahakama ya Tanzania inafanya katika suala zima la Usuluhishi ‘Mediation’ na
masuala mengineyo.
Waziri wa Katiba na
Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi
akizungumza leo na wajumbe
kutoka Taasisi ya Slynn.
|
mjumbe Sean Hichorst wa (pili kulia) akifafanua
jambo na (pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Slynn , Alison Fenney. |
|
wajumbe kutoka
Taasisi Slynn Mhe. Lord Bonomy (wa
kwanza kulia) na ( wa pili kulia )Nic Madge wakimsikiliza Waziri wa Katiba na
Sheria , Profesa Palamagamba Kabudi
(hayupo pichani), alipokuwa anazungumza nao leo
kwenye ofisi ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
|
Msajili Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati akizungumza leo kwenye mkutano wa
Mazungumzo baina ya na Waziri Katiba na
Sheria na ujumbe kutoka Taasisi ya Slynn
yaliyofanyika kwenye ofisi ya Mahakama Kuu ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni