Alhamisi, 3 Januari 2019

KIKAO KAZI CHA KUBORESHA HUDUMA ZA MAHAKAMA YA TANZANIA CHAENDELEA KISUTU



Mtendaji wa Mahakama ya Rufaa, Bw. Solanus Nyimbi akichangia hoja  wakati wa   kikao kazi wa cha  kuboresha huduma  za  Mahakama ya Tanzania. kikao hicho  kinaendelea kufanyika  kwenye Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam. Kikao  kazi  hicho kilianza Januari 2, mwaka huu na  yanatarajia kumalizika Januari 4,mwaka huu.
Baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika kikao  kazi kinachoendelea kwenye Kituo cha Mafunzo  cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Ndani,Bw. Kocheka Kashenge, akimwakilisha Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mahakama ya Tanzania, kuwasilisha mtiririko wa kazi wa eneo hilo wakati wa  kikao kazi  kinachoendelea kufanyika  kwenye Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Mhasibu Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw.  Fanuel Tiibuza akichangia hoja wakati wa kikao kazi hicho.
Afisa Tehama,Bw. Allan Machela akiwasilisha mtiririko wa kazi wakati wa kikao kazi  hicho, kinachoendelea kufanyika kwenye Kituo cha Mafunzo  kilichopo Kisutu jijini Dar  es Salaam.

.
 
 
 
 
Hakimu Mkazi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri, Debora John akiwasilisha mtiririko wa kazi  wa  kurugenzi hiyo wakati  wa kikao  kazi hicho. 
 

  Mkurugenzi Msaidizi wa Ukaguzi na Usimamizi wa Maadili, Bw.Warsha Ng’humbu akichangia hoja wakati wa kikao kazi hicho.
 

Mwenyekiti wa kikao kazi hicho, Bw, Mathias Mwang’u(kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji naMkurugenzi wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano (TEHAMA), Bw. Kalege Enock (kulia)wakisikiliza kwa makini uwasilishaji wa mtiririko wa  kazi wa Mahakama ya Tanzania, wakati kikao kazi kinachoendelea kufanyika kwenye Kituo cha Mafunzo  kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni