Ijumaa, 4 Januari 2019

KIKAO KAZI CHA KUBORESHA HUDUMA ZA MAHAKAMA YA TANZANIA CHAFUNGWA KISUTU LEO


Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti  wa  kikao kazi cha kuboresha huduma  za  Mahakama ya Tanzania,(Business Process) Bw.Mathias Mwang’u  akifunga kikao kazi  hicho cha  siku tatu kilichofanyika katika Kituo cha Mafunzo  kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kikao hicho ni muhimu   kwa kuwa kitaiwezesha Mahakama kutoka hatua moja hadi nyingine yaani  kuingia  kwenye Mahakama Mtandao(e Judiciary).
 
Mkurugenzi wa Kurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri,Mhe. Eva Nkya  akiwasilisha mtiririko  wa kazi  wa kurugenzi  hiyo wakati wa kikao kazi cha kuboresha huduma za Mahakama ya Tanzania.
 
 

Mkurugenzi Msaidizi wa Kumbukumbu za Kimahakama, Bi.Agnes Buyota akichangia hoja wakati wa kikao kazi  hicho  cha  Mahakama ya Tanzania.  

 
 
 

 
 

 
 
 
 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni