Jumatano, 2 Januari 2019

KIKAO KAZI CHA KUBORESHA HUDUMA ZA MAHAKAMA CHAANZA LEO KISUTU


Mtendaji wa Mahakama Kuu,Bw. Leonard Magacha, ambaye amemwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama akitoa neno kuhusu ufunguzi wa kikao kazi cha  Mahakama ya Tanzania. Kikao  hicho kinaendelea kufanyika  kwenye Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam.,ambapo  alimtaka kila mtumishi wa mahakama kuwajibika na kuboresha utendaji wake wa kazi.Kikao  hicho  kimeanza Januari 2,mwaka huu na kinatarajia kumalizika Januari 4,mwaka huu.

 Aliongeza  kuwa  Mahakama ya Tanzania  ipo kwenye utekelezaji  wa Mpango Mkakati iliyojiwekea kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia  mwaka 2015/16hadi 2019/20.Miongoni mwa mambo  yaliyo kusudiwa kuboreshwa ni eneo la utoaji huduma mbalimbali  zinazotolewa na Mahakama. Mpango Mkakati wa Mahakama unazo  nguzo kuu tatu(3) ambazo ni Kuimarisha Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, kuwezesha Upatikanaji  na Utoaji wa haki kwa wakati na kurejesha imani  ya jamii na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za kimahakama.
Alisema  katika mwendelezo wa kuboresha huduma Mahakama inapitia mtiririko wa kazi zake ili  kubaini  mapungufu na fursa zilizopo baina ya wadau ndani na nje ya Mahakama.
Hivyo kupitia kikao kazi hiki  Idara /vitengo  mbalimbali  vya Mahakama vitawasilisha mtiririko wa kazi (Business Process)zao pamoja na matarajio ya kuboresha huduma zake ili kuweza kupata  mpangilio wa kazi wa huduma zitolewazo kwa kila idara.





Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock (kulia)akitoa maelezo kuhusu  kikao  kazi  cha  Mahakama. kikao kazi  hicho cha siku tatu kinafanyika leo kwenye Kituo cha Mafunzo cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam.
 
Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Messeka  Chaba akitoa ufafanuzi kuhusu mtiririko wa kazi(Business process)

Baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika kikao kazi  cha siku tatu kinachoendelea kufanyika  kwenye Kituo cha Mafunzo  cha Mahakama kilichopo Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi  wa Idara ya Ukaguzi wa Huduma za kimahakama, Mhe. Happiness Ndesamburo akichangia jambo  kuhusu  kikao kazi hicho.

 Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Huduma za  Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Bi. Patricia Ngungulu akielezea mtiririko wa kazi , upande wa mafunzo.

Mhe. Kinabo Minja akiwasilisha utendaji wa Idara ya Ukaguzi wa Huduma  za kimahakama wakati wa mafunzo hayo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Erasmus  Uisso akielezea mtiririko wa kazi wa idara hiyo .
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Khamadu Kitunzi akielezea kuhusu mtiririko wa kazi wa kitengo hicho.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Nurdin Ndimbe akielezea mtiririko wa kazi wa kitengo hicho.

(Picha na Magreth Kinabo)


 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni