Jumatano, 16 Januari 2019

UJUMBE KUTOKA TAASISI YA SlLYNN WATEMBELEA MAHAKAMA YA USULUHISHI NA KISUTU.

Jaji Mfawidhi  wa Mahakama ya Usuluhishi,Mhe. John Mgetta  akizungumza leo na ujumbe  wa Taasisi ya Slynn.


Afisa Teknolojia  ya  Habari na Mawasiliano(TEHAMA),Dhillion  Uisso kimwonyesha mifumo ya kusajili kesi Mhe.Nic  Madge  kutoka Taasisi ya Slynn.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya usuluhishi, Mhe. John Mgetta(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka taasisi Slynn , wakiweno viongozi wengine.

Naibu Msajili  wa Mahakama ya Kisutu Mhe. Kevin  Mhina  akizungumza na ujumbe kutoka Taasisi ya Slynn kutoka kushoto  wa kwanza ni Alisan  Fenney na wa pili ni Mhe.Nic Madge. Kulia wa kwanza ni Mhe.Lord  Bonomy na pili ni Joachim Tiganga Naibu  Msajili  Mfawidhi Kanda ya Dar es Salaam.

Naibu Msajili  wa Mahakama ya Kisutu Mhe. Kevin  Mhina  akizungumza na ujumbe kutoka Taasisi ya Sylnn.





 Naibu Msajili  wa Mahakama ya Kisutu Mhe. Kevin  Mhina (kushoto) akimwonesha jalada  la kesi Mhe. Nic Madge (katikati) kutoka Taasisi ya Slynn na  kwanza kushoto ni  Alisan Fenney.


Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto, iliyoko Kisutu jiji Dar es Salaam, MheAgnes Mchome (kulia) akizungumza na ujumbe toka Taasisi ya Slynn , Mhe.Nic Madge (wa kwanza kushoto )na Mhe.Lord Bonomy (wa pili kutoka kushoto).


Na Magreth Kinabo

 Jaji Mfawidhi  wa Mahakama ya Usuluhishi, Mhe. John Mgetta amesema  changamoto inayoikumba mahakama hiyo ni ukosefu  wa mahakimu na majaji wa kutosha.

 Aidha Mhe. Mgetta aliongeza kwamba ukosefu wa wakufunzi wa kutosha au wadau wa usuluhishi, ambao ni mawakili , maafisa kutoka  ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali , wanasheria kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na watumishi wengine wa mahakama  .

Kauli hiyo ilitolewa  jana na Mhe. Mgetta wakati akizungumza na ujumbe kutoka taasisi  ya Slynn  ulifika mahakamani hapo  kwa ajili ya kuangalia mahakama hiyo inavyofanya kazi.

“ Baadhi ya wananchi hawana uelewa kuhusu umuhimu wa  masuala ya usuluhishi na wanafikiri kuwa   kupoteza muda,” alisema Jaji Mgetta.

 Akizungumzia kuhusu  utendaji kazi wa Mahakama hiyo alisema  kuanzia  Julai 2015 hadi  Juni 2018 ilipokea kesi za madai  kwa ajili ya kufanyiwa usuluhishi 563. Kesi 546 zilifanyiwa usuluhishi kati ya  hizo 125 zilifanikiwa kupata usuluhishi na 415  zilishindwa kupata usuluhishi, pia 15 bado zinaendelea kufanyiwa usuluhishi.

Ujumbe huo pia ulitembelea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na Mahakama ya Watoto.

Hakimu Mkazi Mwandamizi  Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto ,Mhe. Agnes Mchome alisema  kuanzia Januari  2018 hadi Desemba walipokea kesi za jinai 118.Pia  katika kipindi hicho  walipokea kesi madai 295.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni