Mahakama ya Tanzania leo imeanza rasmi wiki ya Sheria ambapo wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani watapatiwa Elimu juu ya Masuala mbalimbali ya Kisheria kuanzaia leo hadi Februari 5, 2019. Pichani ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Edward Nkembo akizungumza na mwananchi aliyetembelea banda la Mahakama katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma leo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Ignus Kitusi (mwenye suti) akimsikiliza Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Charles Magesa akimuelezea jambo alipotembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square.
Mtendaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Bwn. Solanus Nyimbi akimuelezea jambo Jaji wa Mahakama yaRufani Mhe. Ignus Kitusi (mwenye suti) kuhusu Maboresho ya Mahakama ya Tanzania alipotembelea Maonesho hayo kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akimuelezea jambo kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo Mwananchi aliyetembelea banda la Mkemia Mkuu katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa Taasisi ambazo ni Wadau wa Mahakama ya Tanzania.
Wananchi wa Dodoma wakipatiwa Elimu kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni