Chuo
cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto inaendesha
Mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na
Wajumbe wa Mabaraza ya Kata kuwajengea uwezo zaidi kiutendaji.
Akifungua
rasmi mafunzo hayo mwanzoni mwa wiki hii katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mheshimiwa Jaji Sam
Rumanyika alioneshwa kuguswa na changamoto mbalimbali zinazokabili Mabaraza ya Kata
zikiwemo ukosefu wa vitendea kazi.
Hata
hivyo Jaji Mfawidhi alifarijika kwa lengo na uwepo wa Sheria ya Mabaraza ya kata
ya mwaka 1985 ambayo ililenga kudumisha suluhu, udugu, utangamano na la zaidi
kwa umuhimu ni kupunguza wimbi kubwa la mashauri yanayosajiliwa katika Mahakama
za mwanzo nchini ambapo kitakwimu ni takriba aslimia 70% ya mashauri ya
husajiliwa kila siku katika mahakama za mwanzo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, aliyekuwa Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na
Ushauri Mhe. Jaji Fahamu Mtulya alisema kuwa mafunzo haya yanalenga kuwawezesha
Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata kupata fursa ya
kubadilishana uzoefu.
“Mbali
na kubadilishana uzoefu Mafunzo haya pia yamelenga kuainisha changamoto katika
utoaji wa haki na kuzitafuatia ufumbuzi ikiwemo kutambua mamlaka zao kwani si
wote wanaofahamu,” alisema Mhe. Jaji Mtulya.
Aliyekuwa
Kaimu Mkuu wa Chuo IJA, Taaluma, Tafiti na Ushauri, Mhe. Jaji Fahamu Mtulya (aliyesimama mbele) akiongoza zoezi la kubadilishana uzoefu baina ya Mjumbe wa Baraza la
Kata (kushoto) na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo.
Sehemu
ya washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Sehemu
ya washiriki wakichangia mada katika mafunzo hayo.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi
na Washiriki wa Mafunzo, (wa tano kushoto) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Mwanza, Mhe. Jaji Sam Rumanyika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni