Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
Hamis Juma amewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma na Maeneo ya jirani kujitokeza
kwa wingi kwenye Maonesho ya Wiki ya utoaji wa Elimu ya Sheria na kutumia
nafasi hiyo kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu Mahakama.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada
ya kutembelea maonesho hayo leo, Jaji Mkuu pia amewataka wananchi wenye
malalamiko na maoni kuhusu utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania kujitokeza na kutoa
hizo ili ziweze kujibiwa na watumishi mbalimbali wa Mahakama walioko kwenye
Maonesho hayo.
Jaji Mkuu pia ameto wito kwa
wananchi wa Dodoma kufika na kuiuliza maswali Mahakama hasa juu ya ucheleweshwaji
wa kesi zao na kuahidi kuwa maswali hayo yatajibiwa kwa lengo la hakikisha wanapata
haki kwa wakati.
“Nawakaribisha wananchi wenye
nafasi kufika kwenye viwanja vya Nyerere Square ili waweze kuona Mahakama ya
Tanzania inavyofanya kazi zake kwa kushirikiana na wadau, ni wakati mzuri wa
kutathmini utendaji wa Mahakama katika kipindi cha mwaka moja yaani tangu 2018”
alisema Jaji Mkuu.
Alisema katika kipindi cha mwaka
mmoja, Mahakama ya Tanzania imepiga hatua hasa kutokana na matumizi ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kesi. Aliongeza kuwa kupitia Maonesho ya Wiki ya
Sheria, wananchi watajifunza kuwasilisha kesi katika ngazi mbalimbali za
Mahakama.
Akizungumzia mashauri kukaa kwa
muda mrefu Mahakamani, Jaji Mkuu alisema Mahakama imekuwa ikilaumiwa
kuchelewesha kesi lakini wakati mwingine kesi zimekuwa zikichelewa kwa kuwa ni
lazima kesi ishughulikiwe na baadhi ya Taasisi wadau huku akitoa mfano kuwa kesi
hupepelezwa na polisi lakini huendeshwa na Mwendesha Mashtaka.
Wiki ya Sheria imeanza jana Januari
31 jijini Dodoma na itamalizika Februari 5 ambapo siku ya Sheria nchini
itaadhimishwa Februari 6, 2019 katika viwanja vya Chimala jijini Dar es salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na Msajili Mkuu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama Wanyenda Kutta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Nyerere Square kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria. Katikati ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania
Mhe. Katarina Revocati.
Wananchi wa Dodoma wakipatiwa huduma kwenye banda la Maonesho la mahakama ya Tanzania lililopo kwenye viwanja vya Nyerere Square.
Mchumi wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Geofrey Mashaffi akifafanua jambo kuhusu Maboresho ya Mahakama hususan ujenzi wa majengo katika banda la kitengo cha Maboresho kwenye kwenye viwanja vya Nyerere Square katika Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la wizara ya Katiba na Sheria kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa kwenye banda la Takukuru kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na Msajili Mkuu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Mahakama Wanyenda Kutta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Nyerere Square kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria. Katikati ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocati.
Meneja wa Kitengo cha Sayansi Jinai na Vinasaba(DNA) wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali bibi Hadija Mwema akifafanua jambo kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipotembelea banda hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni