Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe.Mohamed Chande Othman amewataka
wananchi kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya Wiki ya utoaji elimu ya sheria
yanayoendelea nchini ili kupata elimu na taratibu mbalimbali za Mahakama.
Kauli hiyo imetolewa
leo Februari 02, mwaka huu na Jaji huyo
Mstaafu akiwa mgeni rasmi wa siku ya matembezi ya uzinduzi wa Wiki ya Elimu ya Sheria yanaendelea kufanyika
kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
“ Natoa wito kwa wananchi kujitokeza na kushiriki katika
maonyesho haya kwani kuna mambo mengi
sana yenye manufaa katika maisha yetu ya
kujifunza na kuyafahamu kwa ustawi wa
shughuli binafsi na taifa kwa ujumla,”alisema
Jaji Mstaafu Othman.
Matembezi hayo
yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia barabara ya Ocean hadi kwenye viwanja vya
Mnazi Mmoja.
Kauli mbiu ya mwaka huu
ni “utoaji haki kwa wakati wajibu wa Mahakama na wadau.”
Aidha Jaji Mstaafu huyo
alisisitiza kwamba huduma zinazotolewa
zielekezwe zaidi maeneo ya vijijini kuliko na wananchi wengi wenye uhitaji wa
msaada wa huduma za kisheria.
Mathalani taratibu
ufunguaji mashauri, uendeshaji mashauri rufaa
mamlaka na taasisi zinazohusika
kuwakamata wahalifu, kufanya upelelezi,kuendesha mashauri ya jinai mahakamani,
na taratibu za ufunguaji na uendeshaji wa mashauri ya madai mahakamani.
Kwa upande wake Jaji
Mfawidhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi alisema elimu ya
kisheria itatolewa kwenye vituo vilivyo
mtaani katika Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam.
Maonesho haya yanadhimishwa
nchini katika maeneo mbalimbali na kitaifa
yanafanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa.
Kilele cha Maadhimsho
kitafanyika Februari 6,mwaka huu kwenye viwanja
vya Chimala na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.John Pombe Magufuli.
Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe.
Mohamed Chande Othman (katikati) akiongoza Matembezi maalum ya ufunguzi wa Wiki
ya Utoaji Elimu ya Sheria kwa upande wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Maonesho haya yanaendelea nchini nzima, kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya
Nyerere Square jijini Dodoma na kwa upande wa Dar es Salaam maonesho haya
yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Walioongozana na Mhe. Jaji ni
baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani, Watumishi wa Mahakama pamoja na
Wageni waalikwa.
Picha mbalimbali za Watumishi
wa Mahakama na Wadau wakiwa katika Matembezi maalum ya kuashiria ufunguzi rasmi
ya Maonesho ya Wiki ya Utoaji Elimu ya Sheria kwa upande wa Mahakama Kuu, Kanda
ya Dar es Salaam yaliyofanyika mapema Februari 2 mwaka huu.
Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe.
Mohamed Chande Othman akifungua rasmi Maonesho ya Wiki ya Utoaji elimu ya
Sheria mapema Februari 02, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,
katika hotuba yake, Mhe. Jaji Chande amewataka Wananchi kutembelea Maonesho
hayo ambayo yanaendelea nchi nzima ili waweze kupata elimu juu ya taratibu
mbalimbali za Kimahakama.
Jaji Mfawidhi, Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi akizungumza na Watumishi na
Wageni waalikwa walioshiriki katika uzinduzi rasmi wa Wiki ya Utoaji wa elimu
ya Sheria.
Sehemu ya Watumishi wa
Mahakama kutoka katika ngazi mbalimbali za Mahakama mkoani Dar es Salaam
wakifuatilia sherehe za uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Utoaji wa Elimu
ya sheria.
Meza Kuu wakifuatilia
kinachojiri katika sherehe hizo.
Kwaya ya Mahakama
ikitumbuiza katika sherehe hizo.
Mgeni rasmi, Mhe. Jaji
Mstaafu Chande akipatiwa maelezo kutoka kwa Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, Mhe. Fovo pindi alipotembelea mabanda hayo ili kujuzwa zaidi
huduma zitakazotolewa.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu ambaye pia ni Naibu Msajili, Mhe.Augustine Rwizile (aliyeshika
kipaza sauti) akifafanua jambo kwa Mhe. Mgeni rasmi pindi alipotembelea katika
banda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mhe. Mgeni rasmi
akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na
la Baraza la Usuluhishi (CMA) ambao pia wanashiriki katika Maonesho hayo, Wadau
wengine wanaoshiriki katika Maonesho hayo pamoja na Mahakama Kanda ya Dar es
Salaam ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Baraza la Ardhi la Wilaya ya
Ilala, Polisi n.k.
Mhe. Mgeni rasmi
akizungumza na Waandishi wa Habari waliohudhuria katika sherehe hizo.
Jaji Mkuu msatafu wa
Tanzania (katikati), Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na
Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu walioshiriki katika sherehe
hizo.
Picha ya pamoja kati ya
Mgeni rasmi Wahe. Majaji na baadhi ya Watumishi wa Mahakama- Dar es Salaam.
(Habari na picha na
Magreth Kinabo na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni