Na Magreth
Kinabo
Mahakama ya Kisutu leo imemsikiliza shahidi aliyeko nchini China kwa njia mtandao ‘video conferencing’ katika kesi ya uhujumu
uchumi.
Kesi hiyo namba
28 ya mwaka 2015 imesikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi,Agustine
Rwizile inamkabili raia wa Kichina Royce Lee ambaye anadaiwa kuwa na simu 30 na
nyanya ambazo zinawezesha kupiga simu
nje ya nchi bila kulipa kodi kwa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA.)
Katika kesi hiyo
Shahidi Charles Okanda Nyatenga aliweza kutoa ushahidi wake kwa kutumia njia ya
mtandao,ambapo alisema anafahamu kuwa
Royce ni rafiki na alimsadia kusajili namba
za simu kwa mitandao mitano
.
Nyatenga alipoulizwa na Mwandesha Mashitaka
Faraji Nguka anafahamu vifaa
vilivyokutwa chumbani kwa Royce alikiri
ana vifahamu.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Februari 25,
mwaka huu
.
Hii ni mara ya
pili kwa Mahakama hiyo kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao na ni mara ya kwanza
kusikiliza kesi ya jinai.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni