Na Magreth Kinabo
Waziri wa Katiba na sheria, Mhe. Profesa Palamagamba
Kabudi amewataka watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyoko Kinyerezi Jiji Dar es Salaama kutoa huduma za utoaji haki bila ubaguzi,
rushwa na weledi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri huyo wakati
akizindua, Mahakama hiyo, ambapo alisema imejengwa kwa ajili ya kusogeza huduma karibu
na wananchi. Hivyo wananchi wanapaswa kupatiwa huduma wanayostahili.
“Mahakama hii imengwa kwa ubora na ubunifu na
wapongeza kwa kusogeza huduma karibu na
wananchi. Ninatoa wito tusiyachafue majengo ya Mahakama hii na kutoharibu
miundombinu yake, bali kuyatunza,” alisema Profesa Kabudi.
Aliongeza kwamba Serikali inatambua miundombinu ya
mahakama iliyopo, itaendelea kutenga bajeti
kwaajili ya kuiboresha.
Kwa upande wake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe .Eliezer Feleshi aliwataka
watumishi hao ,kufanya kazi kwa kujituma.
Waziri wa Katiba na
Sheria,Mhe.Profesa Palamagamba Kabudi akizundua Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyoko Kinyerezi jijini Dar
es Salaam.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni