Jengo la Mahakama ya Mwanzo Mkunya, Newala likiwa katika hatua za ukamilishwaji wake. Mradi wa ujenzi wa jengo hili ulianza rasmi Desemba 14, 2018 na utakamilika April 14 mwaka huu. Mkandarasi wa Jengo hili ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na litagharimu zaidi ya shilingi milioni 200.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na wananchi wa Mkunya mara baada ya kuwasili kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa Jengo la
Mahakama ya Mwanzo Mkunya wilayani Newala. Kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mtwara Mhe. Dkt. Fauz Twaib.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akipokea taarifa ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mkunya kutoka kwa Mhandisi wa TBA.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akikagua jengo la Mahakama linaloendelea kukamilishwa.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akifuatilia jambo alipotembelea eneo la ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mkunya. Mwenye koti katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Hussein Kattanga.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea eneo la ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mkunya. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Mzee Hassan Said Likulunga (katikati) ambaye alitoa eneo la ekari 2 kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mkunya. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mtwara Mhe. Dkt. Fauz Twaib.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mtwara Mhe. Dkt. Fauz Twaib na Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo wakiwa katika picha ya pamoja na Mzee Hassan Said Likulunga (wa pili kushoto ) aliyetoa eneo la
ekari 2 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo Mkunya.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa eneo la Mkunya wilayani Newala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni