Na
Lydia Churi- Mahakama-Mbeya
Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wameanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi
wa majengo ya Mahakama ya Tanzania inayoendelea nchini ambapo leo wajumbe hao
wametembelea miradi iliyopo wilayani Rungwe pamoja na Uyole jijini Mbeya.
Pamoja na wajumbe wa kamati
hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya Mhe. Robert Makaramba
pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome pia walikuwa ni
miongoni mwa viongozi walioshiriki kwenye ziara hiyo.
Katika ziara hiyo mkoani
Mbeya, wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walianza ziara
yao kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya wilaya ya Rungwe ambao bado
uko katika hatua za awali.
Mradi huu uliopangwa
kutekelezwa mwaka 2017/2018 unahusisha huduma za mahakama ya wilaya na ya Mwanzo
mjini Rungwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na
kusimamiwa na Chuo kikuu cha Ardhi kama Mtaalamu Mshauri.
Aidha, Mradi wa Ujenzi wa
Mahakama ya wilaya na Mahakama ya Mwanzo Rungwe mjini ulianza kutekelezwa mwaka
jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili mwaka huu.
Baada ya kutembelea
ujenzi wa Majengo ya Mahakama wilayani Rungwe, wajumbe wa Kamati hiyo pia
walitembelea ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Uyole ulioanza kutekelezwa Desemba
2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi April mwaka huu.
Mradi huu unatekelezwa na
Mkandarasi M/S PIM Innovators na kusimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
mkoa wa Mbeya kama Mtaalamu Mshauri. Hatua iliyofikiwa sasa ni kuezeka na
kuanza kazi za umaliziaji (finishing).
Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pia wanatarajia kutembelea na kukagua ujenzi
wa Mahakama katika mkoa wa Arusha na Manyara.
Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Rungwe pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe Mjini likiwa limefikia hatua hiyo ya ujenzi kama ambavyo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea leo.
Jengo
la Mahakama ya Wilaya ya Rungwe pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe
Mjini kama linavyoonekana kwa mbele.
Jengo
la Mahakama ya Wilaya ya Rungwe pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe
Mjini kama linavyoonekana sehemu ya juu.
Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Bwana Khamadu Kitunzi akiwaelezea jambo wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembea ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe leo.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kushoto)akimsikiliza Mhandisi
wa Mahakama ya Tanzania, Bwana Khamadu Kitunzi (hayupo pichani) akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya wilaya ya Rungwe kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembea .Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Mbinga Mhe. Sixtus Mapunda.
Mhandisi
wa Mahakama ya Tanzania, Bwana Khamadu Kitunzi na Mbunge wa Mbinga Mhe. Sixtus Mapunda wakielezea jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
walipotembea kukagua ujenzi wa Mahakama hiyo.
Mhandisi
wa Mahakama ya Tanzania, Bwana Khamadu Kitunzi akimuonyesha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Mchengelwa mchoro wa jengo la Mahakama ya wilaya ya Rungwe.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole likiwa limefikia hatua ya ukamilishwaji
Mkurugenzi wa Mipango wa Mahakama ya Tanzania Bwana Mathias Mwangu akielezea jambo wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo
la Mahakama ya Mwanzo Uyole mkoani Mbeya. Katikati ni Katibu Mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome.
Katibu Mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akielezea jambo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni