Na Mary Gwera, Mahakama
Mahakama
ya Rufani Tanzania, kwa mara ya kwanza,imeendesha jumla ya mashauri nane
(8) kupitia ‘video conference’ iliyofanyika kati ya Dar es Salaam na Mbeya.
Mashauri
hayo yalisikilizwa rasmi kuanzia Machi 11 na Machi 12, kwa nyakati tofauti na jumla ya
Majaji wanne (4) wa Mahakama hiyo ambao ni, Mhe. Jaji Rehema Mkuye, Mhe.
Jaji Sivangilwa Mwangesi, Mhe. Jaji Gerald Ndika na Mhe. Jaji Jacobs
Mwambegele.
Mashauri
yote nane yalikuwa ni maombi ya kuongezewa muda ili kuwawezesha waleta maombi
kufungua rufaa zao katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania nje ya muda.
Aidha, kati ya mashauri yaliyosikilizwa March 12, kupitia ‘Video Conference’ iliyopo katika Kituo cha Mafunzo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na ile iliyopo Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, ilikuwa ni shauri la maombi ya madai kati ya Venance Nyaringa Kazuri na Eldard Mwesiga Sospeter lililosikilizwa na Mh Jaji Jacobs Mwambegele.
Aidha, kati ya mashauri yaliyosikilizwa March 12, kupitia ‘Video Conference’ iliyopo katika Kituo cha Mafunzo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na ile iliyopo Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, ilikuwa ni shauri la maombi ya madai kati ya Venance Nyaringa Kazuri na Eldard Mwesiga Sospeter lililosikilizwa na Mh Jaji Jacobs Mwambegele.
Wadaawa
wote waliokuwa wakiwakilishwa na mawakili waliweza kutoa hoja zao na mwisho Mhe. Jaji aliahidi kutoa uamuzi katika muda
utakaopangwa na Wadaawa wote wa pande mbili watajulishwa.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Jaji Mwambegele alisikiliza pia Shauri lililomhusisha Bi. Agnes Sanga dhidi ya Amon Halinga na
Peter Haonga ambapo Bi. Agness Sanga ameiomba Mahakama hiyo ikubali maombi
yake ya kuongezewa muda ili kusajili rufaa yake nje ya muda.
Kufuatia
hatua hiyo Jaji wa Mahakama hiyo, Mhe. Jaji Mwambegele baada ya kusikiliza
shauri hilo ameahidi kutoa uamuzi katika muda utakaopangwa.
Akizungumzia
faida za Matumizi ya ‘video conference’, Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama ya
Rufani Tanzania, Mhe. Elizabeth Mkwizu aliainisha faida hizo kuwa ni pamoja na
kupunguza gharama za uendeshaji wa mashauri
na kupunguza muda wa usikilizwaji wa
mashauri kwa Mahakama na kwa wadau na pia ni kutekeleza kwa vitendo dira ya
Mahakama ya Utoaji Haki Sawa kwa wote na
kwa wakati.
“Kwa
kawaida, ili kuendesha kesi hizi, tulipaswa kuwasafirisha Wahe. Majaji, na
watumishi wengine kwenda Mbeya na Sumbawanga ambapo mashauri haya yamesajiliwa ambapo
ingelazimu kulipia mafuta ya magari,malazi na stahiki zingine za watumishi ,hali
ambayo inatumia gharama kubwa na hurefusha muda muda wa usikilizwaji wa mashauri,” alieleza Mhe.
Mkwizu.
Mhe.
Mkwizu aliongeza kuwa gharama inayotumika katika uendeshaji wa kesi kupitia
‘video conference’ ni kiasi cha shilingi 140,000/- kwa vituo vyote viwili kwa
siku huku kila kituo kikitumia shilingi 70,000/-. Kwa kawaida kesi hizi
zingesikilizwa kwa njia ya kawaida zingegharimu kiasi kikubwa cha fedha.
Teknolojia
hii ya ‘Video conference’ imewekwa pia katika maeneo kadhaa ambayo ni Mahakama
Kuu-Dar es Salaam, Mahakama Kuu- Bukoba, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
pamoja na Gereza la Keko.
Vifaa
hivi ambavyo tayari vimewekwa na vingine vitakavyowekwa katika Mahakama
zitakazochaguliwa zinalenga kuwezesha uendeshaji wa mashauri na Mafunzo.
Mahakama
ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5)
(2015/2016-2019/2020) imelenga kuboresha huduma zake katika nyanja mbalimbali
lengo likiwa ni kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati kama isemavyo dira yake.
Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Mhe. Jaji Jacobs Mwambegele (aliyeketi katikati) akisikiliza kesi ya
kwa kutumia ‘Video’ conference’ iliyopo katika Kituo cha Mafunzo, Kisutu Dar es
Salaam na iliyopo Mahakama Kuu Mbeya.
Mlalamikaji, Bi Agness Sanga
kutoka Mbeya (analiyesimama katika screen) akitoa utetezi wake mbele ya Mhe. Jaji
Mwambegele.
(Picha na Mary Gwera)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni