Jumamosi, 9 Machi 2019

WATUMISHI WANAWAKE WA MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA ARDHI WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI


Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Joaquine De Mello akitoa mada kuhusu rushwa ya ngono na ‘sextortion’ kwa ujumla, amewaasa Watumishi hao kufanya kazi kwa kujiheshimu huku wakisimamia haki sawa kwa wote kwa kukemea vitendo vya rushwa ya ngono na vitendo udhalilishwaji wa kijinsia.
Picha mbalimbali za Watumishi wanawake wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Kaimu Jaji Mfawidhi alipokuwa akitoa mada katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 08, katika moja ya kumbi zilizopo katika jengo la NHIF Posta jijini Dar es Salaam.





Wakiburudika kwa pamoja katika hafla ya kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ‘The International Women’s Day’ Machi 08.
 Ukataji keki na ufunguaji wa shampeni katika hafla hiyo.

Picha ya pamoja: Katikati ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Joaquine De Mello (katikati), kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, Mhe. Leila Mgonya na kulia ni Jaji wa Mahakama ya Ardhi, Mhe. Salma Mussa Maghimbi wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Watumishi wanawake wa Mahakama ya Ardhi waliohudhuria katika hafla hiyo.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni