Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Dkt. Eliezer Feleshi leo amewasili mkoani Iringa
kuanza rasmi ziara ya kikazi ambapo atakagua shughuli za Mahakama Kuu ya
Tanzania kanda ya Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa
na ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda hiyo, Jaji Kiongozi atakuwepo
hapa mkoani Iringa mpaka mwisho wa wiki, kabla ya kwenda mkoani Njombe.
Mheshimiwa Jaji Kiongozi
alifika mjini Iringa Majira ya saa 5 asubuhi na kupokelewa na viongozi mbalimbali
wa Mahakama kuu kanda ya Iringa wakiongozwa na Jaji Mfawidhi wa kanda hiyo Mheshimiwa
Penterine Kente.
Kwenye ziara yake hii
mheshimiwa Jaji Kiongozi atafanya shughuli mbalimbali za kikazi ikiwemo
kushiriki kumuaga kitaaluma aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya
Iringa mheshimiwa Mary Simbo Shangali, ambaye anaagwa rasmi kesho siku ya
Ijumaa tarehe 5 April, 2019.
Mheshimiwa Jaji Kiongozi katika
ziara yake pia anatarajiwa kuzungumza na watumishi wa Mahakama na kukagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo la Mahakama mkoani humo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akizungumza na Viongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Iringa(hawapo pichani)mara baada ya kuwasili mkoani humo kuanza rasmi ziara ya kikazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni