Jumanne, 2 Aprili 2019

MAHAKAMA KUU KANDA YA DODOMA YAPATA JAJI MFAWIDHI


Na Stanslaus Makendi, Mahakama Kuu Dodoma

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imempokea Jaji Mfawidhi Mhe. Lameck Michael Mlacha ambaye ameripoti kituoni hapo Aprili Mosi, mwaka 2019.

Mhe. Jaji Mlacha amepokelewa na baadhi ya watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Dodoma sambamba na kufanya kikao kifupi na viongozi wa Mahakama Kuu Dodoma, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya Dodoma akiwa na ajenda kuu ya kufahamu hali ya mashauri na Takwimu.

Kabla ya kuripoti Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma,Jaji Mlacha alikuwa ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.


Maoni 2 :

  1. mungu ampe maisha marefu jaji mlacha alikuwa jaji mahakama kuu kanda ya mtwara

    JibuFuta
  2. ni jaji ambaye anachapa kazi kwa weledi mkubwa sana problem solver mpenda haki na mchapa kazi

    JibuFuta