Na Jovian Katundu, Mahakama-Mwanza
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi
Kanda ya Mwanza ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe. Jaji Sam
Rumanyika amewaasa watumishi wa Mahakama kufanya kazi zinazotoa matokeo chanya
kwa wananchi wanaofika Mahakamani kupata huduma.
Akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa
Mahakama Kanda ya Mwanza, kilichofanyika Machi 29,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Geita, Mhe. Jaji Rumanyika alisema kuwa kuna baadhi ya
Watumishi hawatimizi majukumu yao ipasavyo.
“Nawasihi kuacha tabia ya kuhudhuria kazini bila matokeo bali mfike kwa ajili ya
kutekeleza majukumu yenu” alieleza Mwenyekiti huyo.
Aidha, Mhe. Jaji Rumanyika
alisisitiza kuhusu suala la kuondoa mashauri ya mlundikano kuwa bado ni kipaumbele hivyo lazima jitihada
ziendelee kufanyika ili kumaliza mashauri ya aina hiyo yaliopo na kutozalisha
upya mashauri yenye umri mrefu.
Pia amewakumbusha menejimenti
kujenga mahusiano mazuri na watumishi waliochini yao ili kuleta ufanisi
mahala pa kazi.
Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi Kanda ya Mwanza ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Kanda
hiyo, Mhe. Jaji Sam Rumanyika (katikati) akiendesha kikao cha Baraza kilichofanyika
Machi 29, 2019. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Bibi. Lilian Mrindoko na
kushoto ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Mwanza, Bw. Amin Msambwa.
Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mwanza, wakishiriki katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi Kanda ya Mwanza ambaye pia ni Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo, Mhe.
Jaji Sam Rumanyika (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa
Mahakama Kanda ya Mwanza walioshiriki katika kikao hicho, walioketi kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Bibi. Lilian Mrindoko na kushoto ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Mwanza, Bw. Amin Msambwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni