Jumatatu, 1 Aprili 2019

MAHAKAMA YA RUFANI KUSHUGHULIKIA JUMLA YA MASHAURI 29 KATIKA VIKAO VYAKE KANDA YA ARUSHA


Na Catherine Francis - Mahakama Kuu, Arusha

Mahakama ya Rufani Tanzania inatarajia kusikiliza na kumaliza jumla ya mashauri ishirini na tisa (29) katika vikao vyake vilivyoanza rasmi Machi 25, 2019 na kumalizika Aprili 12, 2019.

Vikao hivyo vimefunguliwa rasmi kwa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa heshima ya Mwenyekiti wa vikao hivyo ambaye ni Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Jaji wa Mahakama ya Rufani. 

Kati ya mashauri hayo, 11 ni mashauri ya jinai na 18 ni mashauri  ya madai. Aidha; Mashauri yote 29 yapo kwenye hatua ya usikilizwaji (hearing) ambapo Wahe. Majaji watapata nafasi ya kusiliza mashauri hayo katika kipindi hicho.

Wahe Majaji walioambatana na Mhe. Jaji Mwangesi ni pamoja na Mhe. Jaji Mhe. Jaji Mmilla na Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika.

Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akikagua gwaride maalum kuashiria uzinduzi rasmi wa vikao cha Mahakama ya Rufani mkoani Arusha.

Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika (wa kwanza kushoto) pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha wakishuhudia tukia la ukaguzi wa gwaride lililokuwa likifanyika kuashiria uzinduzi rasmi wa vikao vya Mahakama ya Rufani mkoani Arusha.
(Picha na Ibrahim Mdachi-IJA-Lushoto)
 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni