Akizungumza na
Waandishi wa Habari Aprili 05, 2019 mara baada ya hafla ya kuagwa rasmi
kitaaluma, iliyofanyika Mahakama Kuu Iringa, Mhe. Jaji Mstaafu Shangali alisema
kuwa ni vyema kutekeleza majukumu kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
“Katika usikilizaji wa
kesi ni vyema kumshirikisha Mungu na kusimamia viapo, hivyo tusicheze na mambo
ambayo tumeapa mbele za Mungu tunapotekeleza majukumu yetu,” alieleza Mhe. Jaji
Mstaafu Shangali.
Aidha; Mhe. Jaji
Shangali aliwatia moyo Majaji na Mahakimu Wanawake nchini kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia misingi na sheria zilizopo bila kutetereka.
“Kuwa Jaji mwanamke kwa
nchi zetu za Afrika si kazi rahisi kutokana na baadhi ya mila desturi zilizopo,
kwa hiyo ni vyema wanawake kutekeleza na kusimamia haki bila kutetereka,”
alisema Jaji Shangali.
Kwa upande mwingine,
Mhe. Jaji Shangali alitoa wito kwa jamii kuelewa kuwa pindi unapokuwa na kesi
Mahakamani kuna kushinda au kushindwa, hivyo ni vyema kukubaliana na matokeo.
“Haki sio kushinda bali
ni kupata kile unachostahili, kudai kwamba umenyimwa haki sio lugha sahihi,
lazima upande mmoja utashinda na mwingine utashindwa,” alisema Jaji Shangali.
Kwa upande wake Jaji
Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi aliyeongoza
hafla hiyo alimuelezea Mhe. Jaji Mstaafu Shangali kuwa alikuwa mchapa kazi na mara
zote alisimamia haki.
“Mhe. Jaji Mstaafu
Shangali ni mfano mzuri wa wachapakazi, amefanya kazi vizuri na hadi kufikia
mwisho hakuna jalada lolote la kesi aliloacha bila kukamilisha na huu ni mfano
mzuri,” alisisitiza Mhe. Jaji Kiongozi.
Mhe. Jaji Mstaafu
Shangali, alianza kazi Mahakama ya Tanzania mwaka 1983, ambapo katika utumishi
wake alishika nafasi mbalimbali na hadi anastaafu Mhe. Jaji Shangali alikuwa
Jaji namba. 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania na vilevile Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Iringa, na kufanya jumla ya miaka 35 ya Utumishi wake ndani ya
Mahakama.
Mhe. Jaji Shangali amewashukuru Viongozi na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake.
Mhe. Jaji Shangali amewashukuru Viongozi na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake.
Jaji Kiongozi Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (wa tatu kulia) pamoja
na Majaji wenzake wa Mahakama Kuu wakijumuika kumuaga kitaaluma Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mary Simbo Shangali (wa tatu kushoto).
Naibu Msajili
Mwandamizi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba (kushoto) pamoja na
Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mhe. Agatha Chugulu wakiwa katika
hafla hiyo.
Mwanasheria Mwandamizi
wa Serikali wa Mkoa wa Iringa, Bw. Adolf Maganda (kushoto) pamoja na Wakili wa
Kujitegemea, Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw.
Rwezaula Kaijage (kulia) wakiwa katika hafla fupi ya Kumuaga Kitaaluma Mhe.
Jaji Mstaafu Mary Shangali.
Mtendaji
anayeshughulikia Mahakama za Mwanzo nchini, Bw. Humphrey Paya (kushoto-katikati) pamoja
na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, Bw. Elvin Mwakajinga (kulia) na
sehemu ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Njombe na wageni waalikwa wakiwa
katika hafla ya kumuaga kitaaluma Jaji Mstaafu Shangali.
Jaji Kiongozi, Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi pamoja Wahe. Majaji
wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Wanasheria wa Serikali mkoani Njombe
waliohudhuria hafla hiyo. Wa tatu kushoto ni Jaji Mstaafu wa Mahakama
Kuu, Mhe. Mary Shangali, wa tatu kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Iringa, Mhe. Penterine Kente, wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu
ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul
Kihwelo, wa pili kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Immaculata Kajetan Banzi,
wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Dunstan
Ndunguru na wa kwanza kulia ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Bw.
Adolf Maganda.Wahe. Majaji pamoja na Jaji Mstaafu Shangali wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Msajili wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.
Picha za pamoja na Watumishi wa Mahakama Kuu-Iringa na Njombe.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa aliyepo uhamishoni kuelekea Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mhe. Immaculata Kajetan Banzi (kushoto) akimkabidhi ua kama ishara ya pongezi kwa Mhe. Jaji Mstaafu Shangali (kushoto), anayeshuhudia katikati ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi.
(Habari na Picha: Na Mary Gwera, Mahakama Kuu-Iringa)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni