Jumatano, 22 Mei 2019

BAADHI YA MAJAJI NA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAKISAJILI LAINI ZA SIMU KWA ALAMA ZA VIDOLE


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Ibrahim Juma (katikati) akisajili  laini  ya simu kwa alama za vidole katika kampuni za simu ya Smile, kushoto  ni Mackie Mdachi  na Arnold Ntiga, ambao ni wasajili kutoka kampuni hiyo.Usajili huo umefanyika Mei 22 kwenye ukumbi  namba moja (1) wa Mahakama ya Rufani Tanzania. 
Wahe. Majaji  wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rehema Mkuye (katikati) Mhe. Winfrida Korosso,(kulia) na Mhe. Barke Mbaraka Sehel aliyesimama kushoto kwa Mhe. Jaji Mkuye wakisikiliza maelezo kuhusu usajili laini za simu kwa vidole wakati  wakijisajili zao  leo katika kampuni ya simu ya Halotel.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akisajili laini  ya simu kwa alama za vidole katika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kulia aliyevaa shati la kitenge  ni  Afisa Mauzo wa TTCL, Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi namba moja  wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe, Rehema Mkuye akisajili laini ya simu kwa alama za vidole  katika kampuni ya Halotel. Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi  namba moja wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.Kushoto ni Afisa Usajili wa kampuni hiyo,  Nelson Nyelela.



Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mhe, Augustine Mwarija akisajili laini ya simu kwa alama za vidole  katika kampuni ya  Vodacom. Usajili huo umefanyika leo kwenye ukumbi namba moja  wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.Kushoto ni  anayemsajili ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Vodacom Happiness Shuma.


Baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakisajili laini za simu  kwa alama za vidole 'finger prints' katika kampuni mbalimbali za simu, zoezi hilo la usajili wa simu kwa upande wa Mahakama ya Rufani unatarajia kukamilika Mei 23.
(Picha na Magreth Kinabo)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni